Mji mwingine wa waasi wakombolewa Mali
Wanajeshi wa Ufaransa wanasema wameukomboa mji wa mwisho uliokuwa ngome ya wapiganaji wa kiisilamu
Wanajeshi wa Ufaransa, wanasema
kuwa wamefanikiwa kuingia katika mji wa waasi wa Kidal, ambao ndio ngome
ya mwisho ya wapiganaji hao.
Huu ndio mji wa mwisho mkubwa ambao walilenga kuukomboa kutoka mikononi mwa wapiganaji.
Wanajeshi wa Ufaransa sasa
wanadhibiti uwanja wa ndege wa Kidal, baada ya ndeghe zao pamoja na
helikopta kutua huko usiku wa kumakial leo.
Wapiganaji wa kiisilamu waliriarifiwa tayari kuondoka mji humo na sasa ni wazi kuwa wanajeshi nduio wanaudhibiti.
Majeshi ya Mali na Ufaransa yamekuwa yakiwasaka
waasi hao katima maeneo ya Kaskazini na hata kukomboa miji ya Gao na
Timbuktu bila ya upinzani wowote. .
Ufaransa ambayo ni koloni ya zamani ya Mali,
ilianza harakati za kijeshi mwezi huu baada ya wapiganaji wa kiisilamu
kuonekana kuwa tisho kubwa katika maeneo ya Kusini.
'Kuangamiza Ugaidi'
Msemaji wa jeshi la Ufaransa kanali, Thierry
Burkhard alithibitisha kuwa wanjeshi wa Ufaransa walishika doria katika
eneo la Kidal usiku kucha Kidal".
Wapiganaji wa kiisilamu waliokuwa wandhibiti Kidal
Rais wa mpito wa jimbo la Kidal, Haminy Maiga,
aliambia vyombo vya habari kuwa wanjeshi wa Ufaransa waliwasili kwa
ndege za kijeshi na waliweza kuukomboa mji huo bila makabiliano.
"wanajeshi hao wanashika doria kwa usaidizi wa helikopta''
Mji wa Kidal,ambao uko umbali wa kilomita 1,500
kaskazini mashariki mwa Bamako, hadi ulipokombol;ewa ulikuwa chini ya
udhibiti wa kundi la wapiganaji wa Ansar Dine.
Wapiganaji hao walitoroka Timbuktu ingawa walifaya kitendo cha kulipiza kisasi kabla ya kuondoka.
Hata hivyo, vuguvugu la Islamic Movement of
Azawad (IMA), ambalo hivi karibuni,lilijitenga na makundi mengine ya
wapiganaji, sasa linadhibiti Kidal, ingawa wapiganaji wa Tuareg pia
wanadai kuudhibiti mji huo.

Post a Comment