ad

ad

38 wafariki dunia katika mafuriko nchini Msumbiji

Umoja wa Mataifa umesema kuwa mafuriko yaliyoiathiri Msumbiji yameua watu 38 na kupelekea wengine 150,000 kukosa makazi. 

Marie Conselee Mukangendo Afisa wa Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF ameyasema hayo katika mji wa Chokwe umbali wa kilomita 230 kaskazini mwa Maputo mji mkuu wa Msumbiji. 

Mukangendo amesema dola zisizopungua milioni 15 zinahitajika ili kuwahudumia waathirika wa mafuriko. Ameongeza kuwa hali ya mambo ni mbaya katika kambi zinazowahifadhi watu waliopoteza makazi yao kutokana na kukosekana huduma muhimu za msingi kama vyoo. Itakumbukwa kuwa watu zaidi ya 700 walipoteza maisha kufuatia mafuriko yaliyoikumba Msumbiji mwaka 2000.
Powered by Blogger.