Lulu Diva Adaiwa Kupangiwa Mjengo na Waziri
HUU ni ubuyu wa motomoto kutoka kwa babu Issa wa Zenji. Ukitaka uumung’unye vizuri, lazima ukunje miguu! Ubuyu mtamu uliolifikia Ijumaa Wikienda unaomung’unywa mjini, unadai kuwa waziri mmoja, amempangishia jumba la kifahari, msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ na sasa mambo yote hadharani. Kwa mujibu wa msambaza ubuyu wetu, nyumba hiyo ipo maeneo ya Mbezi-Beach, Dar ambapo waziri huyo amekuwa akiingia nyumbani kwa Lulu Diva kwa siri usiku wa manane.
KUTOKA KINONDONI HADI MBEZI-BEACH
Chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa Lulu Diva kilidai kuwa, awali, msanii huyo alikuwa akiishi maeneo ya Vijana-Kinondoni, Dar. Ilidaiwa kuwa, baada ya kuanzisha uhusiano na waziri huyo, hivi karibuni Lulu Diva alihamishwa Kinondoni na kigogo huyo kwa madai kwamba alikuwa akiishi kwenye msongamano. “Unajua alipokuwa akiishi Lulu Diva mwanzoni kulikuwa ni maeneo ya watu wengi, sasa baada ya kuanza uhusiano na mheshimiwa (waziri) alimuamishia maeneo ya Mbezi-Beach ambako hakuna mazingira ya watu wengi na sasa mtoto anaendelea tu kula upepo wa Bahari ya Hindi,” kilimwaga ubuyu chanzo hicho.
INA KILA KITU
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kwamba, katika nyumba anayoishi Lulu Diva kwa nguvu ya waziri huyo, ina kila kitu ndani ambacho kinamfanya aisitoketoke kama ilivyo kwa mastaa wengine ambao hupenda kuzurura hovyo. “Nyumba ambayo anaishi Lulu Diva ina kila kitu cha thamani. Unaambiwa mtoto sasa atatoka aende wapi? Ametulia tulii…na anaishi maisha ya kistaa tofauti na wasanii wengine,” kiliweka nukta chanzo hicho na kumpisha rafiki mwingine wa Lulu Diva ambaye aliling’ata sikio gazeti hili: “Bidada sasa hivi sponsa ni mheshimiwa waziri kwa hiyo
ana uhakika
wa maisha.”
NYUMBANI KWA LULU DIVA
Baada ya kumwagiwa ubuyu huo na ili ukamilike vizuri, Ijumaa Wikienda lilifunga safari hadi nyumbani kwa Lulu Diva ambapo kweli lilikutana na jumba la kifahari
lililokuwa na kila kitu ndani. Alipoulizwa kuhusu madai hayo ya kupangishiwa jumba hilo na waziri, Lulu Diva aliomba habari hiyo isiandikwe kwenye gazeti. Ijumaa Wikienda: Lulu Diva hapa unapoishi ni pa gharama kubwa mno na kuna ubuyu kuwa umepangishiwa na waziri, je, ni kweli? Lulu Diva: Jamani kwani watu hawaoni siku hizi kama muziki wangu umeanza kuonekana. Ijumaa Wikienda: Kwa hiyo unataka kuniambia ndiyo umeweza kufanya yote haya? Je, hizi habari kuwa, kuna mkubwa serikalini anahusika zikoje? Lulu Diva: (kicheko) hakuna kit u kama hicho…bwana mkubwa gani sasa? Ijumaa Wikienda: Inasemekana (mwandishi anamtajia jina la waziri) ndiye anawezesha yote haya, je, ni kweli? Lulu Diva: Daah… jamani ukiandika hiyo habari itaniharibia hata kwake maana ni mtu ambaye ananisaidia na hapendi mambo yake yajulikane kabisa. Ijumaa Wikienda: Tunashukuru kwa kuwa mkweli. Lulu Diva: Asante ila ninaomba usiniharibie!
WAZIRI VIPI? Jitihada za kumpata waziri huyo hazikuzaa matunda baada ya simu yake ya kiganjani kutokuwa hewani kila ilipopigwa hivyo jitihada zinaendelea.
CHANZO: GAZETI LA IJUMAA WIKIENDA
Post a Comment