Mzozo Syria wafikia kiwango cha kutisha
Mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa
nchini Syria , Lakhdar Brahimi, ameliambia baraza la usalama la Umoja wa
Mataifa kuwa mzozo nchini Syria umefikia kiwango cha kutisha ambacho
hakijawahi kushuhudiwa.
Bwana Ibrahim amesema kuwa Syria inaangamizwa
siku hadi siku kuhu athari kubwa zikiwa ni kwa kanda nzima , na kwamba
baraza la usalama lenye mgawanyiko linapaswa kuchukua hatua .
Alikuwa akitoa mfano juu ya kushindwa kwa baraza
hilo kuafikiana ikiwa rais Assad anapaswa kushirikishwa katika kipindi
cha mpito cha kisiasa au la.
Kauli ya Mjumbe huyo wa Umoja wa mataifa imetolewa saa kadhaa baada ya watu kadhaa kukutwa wameuawa katika mji wa Aleppo.
Imebaini ka kuwa waliuawa wakati mmoja. Serikali
na Upinzani kila upande umekuwa ukimlaumu mwenzake kwa mauaji hayo.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watu elfu 60,000
wamekwishauawa nchini Syria tangu mzozo ulipoanza mwezi March 2011

Post a Comment