HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIYEFUMANIWA
KUFUMANIWA ni tatizo kubwa, msaada usipopatikana haraka madhara
yanaweza kutokea. Kufumania ni mtego, usipotumia busara kuuvuka,
utaharibu harakati zako zote za maisha. Kwa nini umpige uliyemfumania?
Akifa utajitetea vipi mbele ya mkono wa sheria? Ili usiingie katika
matatizo, zingatia nitakayoyasema pale unapomfumania yule umpendaye,
laazizi wa moyo wako. Tuchukulie mfano, wewe ni mwanamme na umemfumania
mkeo, fanya mambo haya.
JAMBO LA KWANZA
Ukiingia wote watashituka. Usipige kelele, tuliza kichwa, usilete papara! Mwambie mkeo atangulie nyumbani. Kisha baki na huyo ‘Jadid’ uliyemfumania na mkeo.
JAMBO LA PILI
Fungua madirisha au washa kiyoyozi kama kipo, ili uliyemfumania apate hewa safi. Kumbuka kwamba usimtishe, mtazame kwa upendo. Kaza moyo!
JAMBO LA TATU
Sema naye kwa upole. Muulize ni kipi kimemfanya ampende mkeo? Je mabinti wote wasioolewa hawaoni hata akafakamia wake za watu? Msikilize zaidi ukimtazama machoni. Kama utaweza, chukua kalamu na karatasi ili unukuu mambo muhimu atakayokueleza.
JAMBO LA NNE
Muulize angekuwa yeye angefanya nini? Kubaliana na kila analosema, usibishane naye, hakuna mshindi katika mabishano. Kipengele hiki kina umuhimu, endapo una ‘tepu rekoda’, rekodi kabisa sauti yake. Pia Usimuite majina mabaya kama, ‘we mzinzi’… tumia maneno mazuri, muite ‘rafiki’. Tafadhali fanya hivyo mzee mwenzangu.
JAMBO LA TANO
Jitahidi upate maji ya uvuguvugu, kisha chukua taulo laini, liloweke na umkande maeneo ya kichwani ukishuka shingoni taratibu. Hii itamsaidia kupunguza hofu aliyonayo. Akitulia, mweleze kwamba hujafurahishwa na kitendo alichofanya. Usisahau kumuuliza kama anajutia kitendo chake… lazima jibu litakuwa ‘ndio’. Mwelekeze mbinu sahihi za kuepuka kuwinda wake za watu na badala yake kama hajaoa, mshauri afanye hivyo hima. Kama yupo kwenye ndoa, basi mshauri atulie na mkewe.
Mfungulie mlango, mpe mkono wa kwa heri ya kuonana ukitabasamu. Akiisha kuondoka, na wewe toka taratibu, nenda nyumbani kacheze na mkeo! Usikubali kuruhusu hasira ikuongoze. katika maeneo nyeti kama fumanizi, busara ndio msingi wa mambo!
SITAKI POVU! NI MAONI YANGU.

Post a Comment