VILLA BOAS AWAKATA MAINI REAL MADRID NA ZIDANE; AWAAMBIA GARETH BALE HANG'OKI SPURS HATA KWA PAUNI MILIONI 60.
KOCHA
Andre Villas-Boas hana shaka Gareth Bale ataendelea kuwa mchezaji wa
Tottenham msimu ujao, akisema kwamba hata itolewe ofa ya Pauni Milioni
60 hatamuuza.
Hot Spur: Gareth Bale brilliance all season has kept Tottenham in the hunt for a top four place
Nyota huyo wa Wales, ambaye leo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari za Kandanda England, amekuwa katika msimu mzuri, akitoa mchango mkubwa kwa Spurs.
Nyota huyo wa Wales, ambaye leo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari za Kandanda England, amekuwa katika msimu mzuri, akitoa mchango mkubwa kwa Spurs.
Akiwa amefunga mabao 19 katika mechi 29
za Ligi Kuu England, Bale ameendelea kuzikuna klabu kubwa, zikiwemo Real
Madrid na Bayern Munich ambazo zinaitaka saini yake kwa gharama yoyote.
Hot Spur: Gareth Bale brilliance all season has kept Tottenham in the hunt for a top four place
Gwiji la Ufaransa, Zinedine Zidane,
ambaye anafanya kazi kama Mshauri Maalum wa vigogo wa Hispania, Real
amesema jana kwamba kiasi cha Pauni Milioni 48, ambazo Madrid waliliipa
Juventus kumpata yeye zaidi ya muongo uliopita, kupata saini ya winga
huyo.
Pamoja na hayo, Villas-Boas amejibu leo,
akisema: "Hata kama kiwango hicho cha fedha kinamlenga mchezaji huyo,
haijalishi kwetu, kwa sababu ni mchezaji wetu na mchezaji ambaye
tunatakiwa kuendelea kuwa naye kuhakikisha tunatimiza malengo yetu na
kuendeleza harakati.
"Taarifa nilizonazo kutoka kwenye klabu
klabu ni kwamba, mchezaji huyo yupo hapa kubaki, hata ikiwa tutapata
nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa au la. Klabu lazima iendelee mbele
kwa kuwashikilia wachezaji wazuri,".

Post a Comment