ALONSO MCHEZAJI WA KWANZA KUSAJILIWA NA MOURINHO CHELSEA.
KOCHA Jose Mourinho yuko tayari kumfanya
Xabi Alonso awe mchezaji wa kwanza kusajiliwa atakaporejea Stamford
Bridge mwishoni mwa msimu kuifundisha tena Chelsea.
Kocha huyo wa Real Madrid alihusishwa
kwa kiasi kikubwa na kurejea Chelsea baada ya timu yake kutolewa katika
Ligi ya Mabingwa Ulaya akihama Bernabeu mwishoni mwa msimu.
Kocha huyo wa Kireno mwenye umri wa
miaka 50 alisema atakwenda sehemu ambayo anapendwa, vyombo vingi vya
habari vikisema Magharibi mwa London, ambako aliifundisha Chelsea
akiibebesha mataji matatu kabla ya kuondoka mwaka 2007 ndiko anakopendwa
zaidi.
Huku kuelekea Chelsea: Jose Mourinho atahamia na Xabi Alonso na London
Unaondoka Jose? Alonso (kulia) inaaminika yuko kwenye mipango ya Mourinho, akihamia Chelsea mwishoni mwa msimu
Inafahamika kwamba Mourinho tayari
amemtambulisha nyota huyo wa zamani wa Liverpool kama mmoja wa wachezaji
atakaowasajili ikiwa atakwedna kurithi mikoba ya Rafa Benitez.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 wa
kimataifa wa Hispania, ambaye alitwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na
Liverpool mwaka 2005, atamaliza mkataba wake msimu ujao na bado
hajakubali ofa ya nyongeza ya mkataba wa miaka kuendelea kuishi Madrid.
Kwa mujibu wa gazeti la Independent,
Alonso ni mmoja kati ya marafiki wa karibu wa Mourinho ndani ya Real na
amesitisha uamuzi wake hadi ajue nani atarithi mikoba ya Mreno huyo.
Akihamia Chelsea, dhahiri atawaumiza mashabiki wa Liverpool, kwani aliwahi kusema atakaribisha ofa ya kurejea Anfield.
Wazi pia akihamia Stamford Bridge
itakuwa utata kati yake na kiungo wa England, ambaye pia ni swahiba wa
Mourinho, Frank Lampard aliyekubali kuongeza mkataba wa mwaka mmoja.
Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Rademel
Falcao, waakti huo huo inaaminika ni mchezaji anayetakiwa zaidi The
Blues, ingawa kuna mchuano mkali na klabu nyingine, Manchester United na
Manchester City kuwania saini ya Mcolombia huyo.

Post a Comment