GODBLESS LEMA: NIMEAGA FAMILIA YANGU IWE TAYARI KUPOKEA MWILI WAKE AKIWA AMEKUFA,ATAENDELEA KUPIGANIA HAKI.
MBUNGE wa
Arusha Mjini Godbless Lema, amesema tangu alipoamua kupigania haki za
wananchi Mbunge wa Arusha Godbless Lema (kushoto), akihutubia maelfu ya
wakazi wa mji wa Arusha na vitongoji vyake katika viwanja vya Shule ya
Msingi Ngarenaro.
Arusha alikwisha itaarifu familia yake kuwa iwe tayari kupokea mwili wake akiwa amekufa.
Lema alisema maneno hayo jana jioni katika viwanja vya shule ya
Msingi Ngarenaro, wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa Arusha katika
kile alichoita kutoa ufafanuzi wa tukio la yeye kuhusishwa na vurugu
zilizotokea katika Chuo cha Uhasibu wiki iliyopita."
Familia yangu, inafahamu na
nilishaiarifu, kwa sababu napigania haki za wananchi, wawe tayari
kupokea maiti yangu na si mgonjwa mwenye majereha," alisema.
Mbunge huyo, alitumia muda
mwingi kumshambulia kwa maneno makali Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa
Mulongo kama ndiye tatizo kubwa la demokrasia mkoani hapa.
"Mulongo akishirikiana na polisi, walijaribu kutengeneza kesi ya mauaji ya yule kijana ti mimi nilihusik
a,lakini kwa sababu nilishaandaa mikanda ya video nakuisambaza wakashindwa,
"Nilishajua nia yao,ndio maana
nikatengeneza ile video na kuisambaza kama sivyo wangenipa kesi ya
mauaji,nasema huu ni mpango wa Serikali kutaka kumpiga mchungaji wa
kondoo ili kondoo watawanyike"
Aliishutumu vikali ofisi ya Bunge kwa kushindwa kukemea utaratibu uliotumiwa na polisi kumkamata.
"Nimedhalilishwa na
kudhalilishwa kwangu ni ninyi mmedhalilishwa,kutukanwa mimi ni ninyi
mmetukanwa,hawakuja na kibali cha Spika, wamekuja kama wanavamia nyumba
ya mhalifu"
Lema alitumia mkutano huo,
kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza uchaguzi katika kata
ya Sombetini, ili kuwapa fursa wananchi kupata kiongozi wao.
"CCM kupitia tume iache uhuni
huu kwa hofu kuwa tukishinda tutaunda halmashauri ya jiji kwa kumtoa
meya aliyepo,nawaambia hatutakubali,ama tutafia barabarani au tutazuia
mahakamani,hii haikubaliki"
"Sheria inasema diwani
asipohudhuria vikao vitatu sio diwani tena (Alphonce Mawazo), aliyekuwa
diwani Sombetini kupitia CCM, alijiunga nasi tangu mwaka jana ,hawa watu
hawako makini hata kidogo"
Katika hatua nyingine,
aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Vijana wa CCM Mkoa wa Arusha
ambaye sasa ni kada maarufu wa Chadema, James Millya amemfungulia mlango
wa kutokea mbunge wa Simanjiro, Christofa Sendeka (CCM).
Millya alidai mwaka 2015,
Simanjiro itakuwa jimbo la Chadema na Mungu akimweka hai na akipitishwa
na chama chake njia ni nyeupe kwake.
"Simanjiro ni yetu,namtaarifu
kuwa 2015 tutashinda kwa kishindo na si hapo tu lengo letu la msingi ni
kuchukua dola" alisema
CHANZO TANZANIA DAIMA

Post a Comment