Je uwezo wa hospitali ya Taifa Muhimbili umeshuka?
.jpg978515054.jpeg)
Muhimbili ni hospitali ya rufaa ya taifa la Tanzania. Hospitali ambayo
inatoa huduma ya juu katika katika sekta ya afya. Lakini siku za
karibuni kumekuwepo na mijadala katika mitandao mbalimbali ya kijamii
juu ya uwezo wa hospitali hii ya taifa. Mijadala hii iliibuka baada ya
mkurengezi wa bmakosa ya jinai bwana Robert Manumba kuamia hospitali ya
Aga Khan toka Muhimbili alipokuwa anatibiwa awali. Watu walihoji iwapo
Muhimbili inatowa rufaa kwenda Aga khan. Jibu ni hapana.
Kiwango cha taaluma walichonacho madaktari wa Muhimbili ni kikubwa. Tena
wengine ni wasomi waliobobea na maprofesa. Hivyo si kweli kwamba uwezo
wa muhimbili umeshuka.
Ikumbukwe kuwa mgonjwa ana haki au matakwa ya kutibiwa hospitali yoyote
nyingine anayotaka. Hii inategemea mfumo wa jamii ulipo. Sekta ya afya
haina tofauti na sekta nyingine mfano elimu na ajira katika nchi yetu.
Mojawapo ya madai ya madktari katika migomo iliyopita ni kuboresha
huduma za afya na kupunguza rufaa zisizokuwa na umuhimu nje ya nchi. Hii
itasaidia kuokoa maisha ya watanzania wengi wasiokuwa na uwezo na hata
kupunguza gharama kutoka kwa wafadhili na serikali ya kupeleka wagonjwa
nje na kuwekeza katika sekta nyingine. Ni ajabu kama utampa mgonjwa
mwenye malaria rufaa kwenda india kutibiwa. Je utatoa rufaa ngapi kwa
mwaka?
Nani asiyefahamu hali ya hospitali zetu nchi. Hospitali nyingi
zinawataalamu wachache na hazina vitendea kazi vya kutosha. Hospitali na
vituo vya afya nchini viko katika hali mbaya. Hivyo watanzania wengi
wanapoteza maisha hata kwa magonjwa ambayo yako katika uwezo wa
wataalam.
Madaktari katika hospitali ya Taifa na hospitali nyingine wamekuwa
wakifanya kazi katika mazingira magumu. Wengine wamekuwa hawautumii
utaalamu wao ipasavyo. Hii imepelekea wengine kwenda nje ya nchi ambako
watatumia ujuzi wao kwa malipo stahiki. Tanzania ni nchi ambayo
wataalamu wake hawathaminiwi. Hivyo si kweli kwamba uwezo wa hospitali
yetu ya taifa umeshuka.
Ni wajibu wa serikali kuhakikisha inaboresha mfumo wa afya. Lazima
kuingoza vitendea kazi na kuboresha maslahi ya wafanyabkazi wake.
Chanzo cha habari na www.paulmasua.com
Post a Comment