Global yatoa mifuko 100 ya saruji ujenzi sekondari Kinondoni
Mifuko hiyo imekabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, na mwakilishi mwandamizi wa Global, Elvan Stambuli, katika ofisi yake iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam.
“Nikiwa mwakilishi kutoka Global Publishers, ninakabidhi mifuko 100 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa sekondari kwa Wilaya ya Kinondoni kutokana na kuguswa na wito wa mkuu wa wilaya hii alioutoa kwa makampuni na taasisi mbalimbali kusaidia kuongeza shule saba za sekondari wilayani Kinondoni ili vijana waweze kupata elimu vizuri,’’ alisema Stambuli.
Wakati huohuo, naye mwakilishi kutoka kampuni ya Ubapa Limited, Wenceslaus Rwezahula, na mwakilishi wa Oyster Bay Pharmacy, Kefa Kijo, walitoa mifuko ya saruji kuchangia ujenzi huo.
Hata hivyo mara baada ya makabidhiano hayo, Makonda aliishukuru Kampuni ya Global Publishers kwa kuchangia mifuko 100 akisema ni mfano wa kuigwa kwa makampuni mengine, huku akisisitiza kuwa bado taasisi na makampuni mengine yanayo fursa ya kuendelea kuchangia ujenzi huo.
PICHA/HABARI: DENIS MTIMA/GPL
Post a Comment