Waziri Lukuvi Asitisha Zoezi la Bomoa Bomoa Dar
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini, Mhe. William Lukuvi
amesitisha zoezi la bomoabomoa kwa muda wa siku14 katika maeneo ya
mabondeni na yaliyovamiwa na kujengwa kinyume cha sheria ili kutoa
nafasi kwa watu waliojenga katika maeneo hayo kuondoa wenyewe mali zao.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi imebainisha kuwa zoezi la bomoa
bomoa limesimamishwa kwa muda kuanzia tarehe 22/12/2015 hadi 05/01/2016.
Taarifa
hiyo imeongeza kuwa eneo la mto msimbazi ni eneo hatarishi na ujenzi
katika eneo hilo ni kinyume na sheria ya mipango miji na 8 ya mwaka 2007
na sheria ya mazingita na.4 ya mwaka 2004.
Maeneo
mengine ambayo serikali imepiga marufuku ni maeneo ya wazi, kingo za
mito, fukwe za bahari, maeneo ya hifadhi za barabara na maeneo
hatarishi.
Aidha,
katika Jiji la Dar es Salaam maeneo ya wazi takribani 180 yamevamiwa
ambayo ni kama ifuatavyo; Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni maeneo 111,
Halmashauri ya Ilala maeneo 50 na Halmashauri ya Temeke maeneo 19.
Post a Comment