Masogange afungukia mimba ya Davido
Video queen maarufu Bongo, Agness Jerald ‘Masogange’ amefungukia taarifa zinazoendelea kuenea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii pamoja na mitaani kwamba amedungwa mimba na mwanamuziki ‘chakaramu’ kutoka nchini Nigeria, David Adedeji Adeleke ‘Davido’.
Akizungumza na mwandishi wetu, Masogange anayesifika kwa kuwa na umbo matata, alikanusha vikali taarifa hizo na kuongeza kuwa anashangazwa sana na watu wanaoendelea kumzushia wakati hana uhusiano naye wa kimapenzi.
“Hivi unajua mimi nashangaa sana kuhusu maneno ya mimi na Davido! Anawezaje sasa kunipa mimba jamani wakati hatuna uhusiano wa kimapenzi? Hiyo mimba inapitia wapi? Watu wanahisi tu kwamba nina uhusiano na Davido lakini siyo kweli na hakuna mwenye uhakika kuhusu hilo,” alisema Masogange.
Mrembo huyo alienda mbele zaidi kwa kueleza kuwa yeye ana mtu wake ambaye hata kama angebeba mimba yake asingekuwa na tatizo lolote lakini kuhusu Davido watu wanaotabiri suala hilo watasubiri sana kwa sababu hakuna ukweli wowote.
“Unajua watu wengi wanapenda sana mambo ya utabiri lakini kwa Davido utabiri wao umegonga mwamba kwa kuwa hana uwezo huo kabisa wa kunipachika mimba kwa sababu sina uhusiano naye wa kimapenzi, labda angekuwa mwanaume wangu hapo nisingepinga,” alisema Masogange.
Licha ya mara kwa mara Masogange kukanusha taarifa za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Davido, vipo viashiria vinavyoonesha kwamba wawili hao wanatoka kimapenzi.
Post a Comment