Baada ya kuachika mara 3 Dida ndoa ya 4!...Avalishwa pete, ajiandaa na sherehe
Na Imelda Mtema Mtangazaji wa Radio Times FM ya jijini Dar es Salaam, Khadija Shaibu ‘Dida’ anatarajiwa kufunga pingu za maisha siku chache zijazo na mwanaume ambaye mwenyewe hakupenda kumtaja jina, hii ikiwa ni mara yake ya nne kufunga ndoa.
Khadija Shaibu ‘Dida’ akiwa na pete ya uchumba aliyovishwa.
Akizungumza na mwandishi wetu muda mfupi baada ya kuvalishwa pete ya
uchumba, Dida anayetangaza Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani, alisema kwa
mwanamke kuolewa ni bahati, hivyo anajihesabu kuwa miongoni mwa wanawake
waliojaliwa kuwa na kismati.
Dida akiwa na aliyekuwa mumewe Gervas Mbwiga ‘G’.
“Unajua kuna watu wanaweza kusema kuwa mimi naolewa hovyo lakini
hawajui siku zote kuolewa ni bahati jamani, kama mtu huna hiyo bahati
unawezaje sasa kupata mume? Haiwezekani kabisa,” alisema Dida na
kuongeza kuwa siku zote watu hawahesabiwi ndoa ngapi wamepitia bali
wanahesabiwa wamepitia vyuo vingapi hivyo ni jambo la kumshukuru Mungu.
Dida na Ezden Jumanne.
Kabla ya kuvalishwa pete hivi karibuni, Dida aliwahi kuolewa na Juma
Mchopanga ‘Mchops’, Gervas Mbwiga ‘G’ kabla ya kuolewa na mtangazaji
mwenzake, Ezden Jumanne Ntambi ambaye walishindwana na kusababisha ndoa
hiyo kuvunjika kutokana na migogoro ya mara kwa mara.Chanzo: Risasi Jumatano
Post a Comment