NANI MTANI JEMBE KITANUKA TAIFA LEO SAA KUMI JIONI
Mchezaji wa Yanga, Kpah Sherman.
KOCHA Mkuu wa Simba, Mzambia, Patrick Phiri, amekiangalia kikosi chake kwa makini na ghafla akachukua maamuzi magumu ya kuwaanzisha wachezaji wapya wawili waliotua kwa ajili ya majaribio, kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe.
Wachezaji hao waliotua Jumatano kwenye kambi yao waliyoweka huko Unguja, Zanzibar ni Simon Sserunkuma, 18, aliyetokea Express na Juuko Murushid aliyekuwa anaichezea Victory University Sports Club, zote za Uganda.
Mchezaji wa Simba, Emmanuel Okwi.
Hiyo ni baada ya wachezaji hao kuliridhisha benchi la ufundi la timu
hiyo kwa uwezo wao uwanjani kwa muda wa siku mbili walizofanya mazoezi
na kikosi hicho cha Phiri kilichorejea jana Ijumaa jijini Dar es Salaam
tayari kwa mchezo wa Nani Mtani Jembe watakaocheza dhidi ya Yanga
inayofundishwa na Mbrazili, Marcio Maximo.Katika mazoezi ya mwisho yaliyofanyika Alhamisi jioni kwenye Uwanja wa Amaan, Unguja, Zanzibar kocha huyo alionekana kuwaanzisha wachezaji hao kwenye kikosi cha kwanza atakachokitumia katika mechi dhidi ya Yanga.
Mshambuliaji, Danny Mrwanda.
Kikosi hicho atakachokitumia leo kwenye mechi dhidi ya Yanga,
kinatarajiwa kupangwa kama ifuatavyo; Ivo Mapunda, Nassoro Said
‘Chollo’, Issa Rashidi ‘Baba Ubaya’, Hassani Isihaka, Murushid, Jonas
Mkude, Ramadhani Singano, Awadhi Juma, Elias Maguli, Simon na Emmanuel
Okwi.Mzambia huyo, katika mazoezi ya jana, alionekana akiwapa maelekezo na mbinu mbalimbali za kucheza wakati timu yake itakapovaana na watani wao wa jadi, Yanga.
Wakati akitoa maelekezo kwa kikosi hicho alichokichagua, mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Mganda, Dan Sserukuma, yeye alikuwa amekaa pembeni ambapo ilielezwa straika huyo hayupo fiti kwa ajili ya mechi hiyo kutokana na kukaa nje ya uwanja kwa muda bila ya mazoezi baada ya Ligi Kuu ya Kenya kumalizika.
Wachezaji hao wawili bado wapo kwenye majaribio kwa ajili ya kusajiliwa na timu hiyo, licha ya kuwepo taarifa za nyota hao raia wa Uganda, huenda wakasajiliwa wakati wowote ule baada ya kuonyesha viwango vikubwa katika mazoezi ya siku hizi mbili.
Mchezaji wa Simba, Mganda, Dan Sserukuma.
Wakati Simba ikitarajiwa kuwa na sura hizo mbili katika usajili wa
dirisha dogo, watani wao wa jadi nao wanatarajia kuwaonyeshea nyota wake
wapya waliowasajili ambao ni kiungo mkabaji Mbrazili, Emerson De
Oliviera na mshambuliaji, Danny Mrwanda aliyetokea Polisi Morogoro.Kutokana na presha iliyopo kwenye mchezo huo kuanzia kwa makocha, wachezaji waliokuwepo tangu msimu uliopita na wale wapya tumuachie Mungu fanye majaaliwa yake.
Post a Comment