WAARABU WAMCHENJIA OKWI KWA BLATTER
KLABU ya Etoile du Sahel ya Tunisia imewasilisha barua ya kurasa
tatu Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) ikimtaka mshambuliaji wa
Yanga, Emmanuel Okwi awalipe Dola 1.3 milioni za Kimarekani ambazo ni
zaidi ya Sh 2 bilioni za Tanzania kama fidia.
Etoile kwenye barua hiyo ambayo Mwanaspoti ina
nakala yake, imewasilishwa Fifa na klabu hiyo inataka ilipwe fedha hizo
za fidia baada ya mchezaji huyo kuvunja mkataba wake na klabu hiyo
kinyume na sheria za Fifa na wakaenda mbali zaidi kwa kusisitiza kuwa
mchezaji huyo kuna watu walimrubuni.
Gharama hizo ni pamoja na fidia za uhamisho,
mshahara wa Juni mwaka jana, mshahara wa kuanzia Julai mwaka jana hadi
Juni 2016, posho zake za kuanzia Julai 2013 hadi Juni 2016, gharama za
malazi, gharama za tiketi ya ndege, gharama za usafiri wa gari, mshahara
wa miezi mitano aliolipwa, pamoja na gharama za kiinua mgongo baada ya
kumaliza mkataba na Etoile.
Barua hiyo ambayo Katibu Mkuu wa Etoile, Adel Ghith aliipeleka Fifa kama utetezi wao kwenye kesi dhidi ya Simba na Okwi, pia aliitoa kwa Simba ikionyesha kuwa Okwi anatakiwa kuilipa Etoile zaidi ya billioni mbili za Kitanzania.
Ghith alisema: “Ni tabia mbaya iliyofanywa na Okwi ambayo haiwezi kuvumilika na hivyo ninaomba Fifa mtupe muongozo kwani mchezaji huyo amevunja mkataba bila kufuata utaratibu na kwa njia isiyokubalika kisheria, tena tunaomba fidia ya gharama kama ifuatavyo.
“Fidia ya gharama za usajili Dola 247, 142 (sawa na Sh 393.6 milioni ),mshahara wa Mei hadi Juni 2013 ambao ni Dola 10,000 (sawa na Sh 15.9 milioni),mshahara wa Julai 2013 hadi Juni 2016 ambazo ni Dola 180,000 (Sawa na Tsh 293 milioni) na posho Dola 480,000 (sawa na Sh 764.5 milioni) kuanzia Julai 2013 hadi Juni 2016.
“Gharama nyingine ni kodi ya miezi 38 ambayo ni Dola 19,000 (sawa na Sh 30.2 milioni), tiketi za ndege za Dola 12,000 (sawa na Sh 19.1 milioni), usafiri wa ndani (gari) Dola 26,600 (sawa na Sh 42.3 milioni), mshahara uliolipwa kwa miezi mitano ya awali Dola 50,000 (sawa na Sh 79.6 milioni), pamoja na kiinua mgongo ambacho angepewa baada ya kumaliza mkataba na Etoile cha Dola 300,000 (sawa na Sh 477.8 milioni),” alieleza.
Barua hiyo ya Etoile imeambatanishwa na nakala sita za muhimu ambazo ni mkataba wa Okwi na Etoile, maelezo ya Fufa (Shirikisho la Soka Uganda), nakala ya ratiba za mazoezi na michezo ya klabu, nakala iliyotafsiriwa kwa Kiingereza yenye ratiba za mazoezi na michezo ya klabu hiyo, barua ya mchezaji ya kujiunga na klabu pamoja na Leseni ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya mchezaji.
Ghith alieleza kwenye barua hiyo kuwa: “Tulifurahi
kuona Okwi akifanya kazi yake vizuri, alifanya hivyo mwanzoni kabla ya
kubadilika lakini alikuwa akishiriki shughuli zote za timu ikiwemo hata
kukichezea kikosi cha U-23 cha klabu hiyo.
“Alikuwa akilipwa mshahara wake kwa kipindi chote alipokuwa na timu na hivyo alikuwa akilipwa kwa mujibu wa taratibu za Fifa na zile za Shirikisho la Soka Tunisia,” alisema Ghith kwenye barua hiyo.
Ghith katika barua hiyo pia alisema: “Ghafla mwezi
Mei Okwi alibadilika na hata kushindwa kuhudhuria na kujiunga na timu.
Alianza kukosa mazoezi lakini bado tulipeleka jina lake kwa ajili ya
mashindano ya Shirikisho Afrika lakini baadaye aliondolewa.
“Baada ya kuwa hivyo, alipoacha kucheza kuna
malipo alikuwa akilipwa kama mchezaji wetu lakini kuna mengine
tulisitisha na tukamwambia kuwa hatutaweza kumlipa kutokana na sheria za
Shirikisho la Soka la Tunisia kwamba mchezaji atalipwa baadhi ya malipo
pale tu anaposhiriki mchezo.
Lakini pia tuliwasiliana na shirikisho letu la Tunisia pamoja na Fufa lakini mchezaji (Okwi) hakutaka kuwasiliana na sisi ili kumaliza matatizo.
Ghith alimalizia kwa kusema: “Tunadhani alishawishiwa na akaamua kuvunja mkataba kwa njia isiyo sahihi na hivyo kutokana na matukio yote hayo ndiyo maana tulichelewa kumlipa mshahara wake lakini pia tulimpa tu kumpendelea kwani hakustahili kulipwa.”
“Tulipokea barua ya Fufa kumualika Okwi kwa ajili ya mchezo wa
kufuzu Kombe la Dunia Brazil 2014 dhidi ya Liberia na Angola, michezo
ambayo iliandikwa kwenye barua kuwa ingeanza tarehe 8-15 Juni 2013
lakini tuligundua kuwa Mei 20, 2013 Okwi tayari alikuwa Uganda bila
ruksa maalumu wala makubaliano yoyote na klabu.
Lakini pia tuliwasiliana na shirikisho letu la Tunisia pamoja na Fufa lakini mchezaji (Okwi) hakutaka kuwasiliana na sisi ili kumaliza matatizo.
“Tarehe 12 Julai mwaka jana, tuliwasiliana na Fufa
na mchezaji ili tuje kumaliza matatizo na pia kumwonyesha utaratibu
pamoja na jinsi mkataba wake ulivyo lakini hakutaka kusikia lolote,”
alisema Ghith kwenye barua hiyo.
Ghith alimalizia kwa kusema: “Tunadhani alishawishiwa na akaamua kuvunja mkataba kwa njia isiyo sahihi na hivyo kutokana na matukio yote hayo ndiyo maana tulichelewa kumlipa mshahara wake lakini pia tulimpa tu kumpendelea kwani hakustahili kulipwa.”
CHANZO NI MWANASPORT

Post a Comment