TAIFA STARS YAPATA SARE DHIDI YA WENYEJI NAMIBIA
Taifa Stars
imefanikiwa kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji wake Namibia katika mechi
ya kirafiki iliyochezwa leo jijini Windhoek.
Stars ndiyo
ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na kiungo mwenye kipaji wa pembeni wa
Azam FC, Hamis Mcha maarufu kama Vialli.
Vialli alifunga bao hilo zikiwa zimebaki dakika tatu tu mpira kwisha, lakini wenyeji wakasawazisha katika dakika za nyongeza. Bao lao lilifungwa katika dakika ya 90+4.

Post a Comment