Samwel Sitta.
Hatimaye
mzee wa "Standards and Speed", Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), Samwel
Sitta, ambaye pia ni Waziri wa Ushirikianmo wa Afrtika
Mashariki, amepitishwa na chama chake, kuwa mgombea pekee wa nafasi ya
Uenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba.
Taarifa
kutoka Dodoma zilizonukuliwa na vyombo vya habari mapema Jumanne
Asubuhi Machi 4, 2014, Samwel Sitta, spika mstaafu anayeelezwa kuleta
mabadiliko makubwa ndani ya bunge la Muungano la vyama vingi, atasaidiwa
na Samia Suluhu Hassan, ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais, anayeshughulikia masuala ya Muungano.
Taarifa
hiyo ilisema, hatua ya Samwel Sitta kuteuliwa kuwa mgombea pekee wa
nafasi hiyo, inafuatia vikao virefu vya wabunge wa CCM vya kimkakati,
ambapo aliyekuwa akitajwa kuwania nafasi hiyo, sambamba na Sitta, Mbunge
wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge alitangaza kujitoa.
Sitta sasa atapambana na wagombea kutoka upande wa upinzani, na haitarajiwi kushindwa.
Umaarufu
wake, ulitokana na falsafa yake ya “Standard and Speed” ambapo, alitoa
fursa karibu sawa kwa wabunge wote kutoka upinzani na chama chake,
wakati wa kuchangia mijadala mbalimbali hata ile iliyoonekana kukibomoa
chama chake.
Kuteuliwa
kwake, kunatarajiwa kulichangamsha bunge hilo maalum la Katiba ambalo
wachambuzi wa mambo wanabashiri kuwa litakuwa gumu mmno kuliongoza,
kwani kuna wajumbe wake, wanatoka kada mbalimbali na hivyo kulifanya
kuwa ni bunge litakalohitaji busara na uvumilivu kuliongoza. |
Post a Comment