MANCHESTER UNITED YAMVUMBUA CRISTIANO RONALDO MPYA …NI KINDA WA SPORTING LISBON, YAMTENGEA £20M
MANCHESTER United imemvumbua Cristiano Ronaldo mpya – kinda wa miaka 19 kutoka Sporting Lisbon ya Ureno anayekwenda kwa jina Carlos Mane (pichani juu kulia). Sporting Lisbon ndiyo timu ya zamani ya Ronaldo kabla ya kutua United kwa ada ya pauni milioni 12.
United inajiandaa kuifumua timu yake huku ikiwa na fungu la pauni milioni 200 kwaajili ya shughuli hiyo ya kusaka nyota wapya.
Mane ambaye anaweza kucheza wing zote mbili au katikati anachukuliwa na klabu yake kama kipaji bora tangu kuondoka kwa Ronaldo mwaka 2003.
Sporting wanatajwa kuwa watahitaji angalau pauni milioni 20 kwa Mane, kiwango kinachotajwa pia kwa kiungo mwingine wa timu hiyo anayewaniwa na Manchester United William Carvalho (pichani chini kushoto).
Kiasi hicho kinaonekana si tatizo kwa Manchester United ambayo kama itauza baadhi ya wachezaji wake basi bajeti yao ya usajili inaweza kuongezeka hadi pauni milioni 300.

Post a Comment