Vijana washauriwa kuwa wabunifu
VIJANA nchini wametakiwa kuhakikisha wanatumia muda wao kufanya
kazi na kubuni miradi mbalimbali badala ya kukaa vijijini wakisubiria
ajira au wafadhili.
Wito huo ulitolewa na mkurugenzi wa kampuni ya Remapt’s Busness
Co.Ldt, William Mligo, alipozungumza na waimbaji wa nyimbo za Injili
pamoja na nyimbo za kijamii mjini hapa.
Mligo alisema vijana wengi wamekuwa na tabia ya kukaa vijiweni
wakiomba misaada au kuendelea kulaumu badala ya kutumia muda wao kubuni
miradi, ili kujikwamua na umaskini.
“Vijana wenzangu huwezi kuondokana na umaskini kama hutakuwa mbunifu.
Ni lazima ufanye kazi na ukisha kuwa na pa kuanzia ndipo sasa unapoweza
kutafuta wafadhili au kujiunga katika kikundi na kuwasilisha andiko kwa
taasisi mbalimbali, ili kuomba msaada wa ufadhili,” alisema Mligo.
Aidha alisema licha ya kampuni yake kuwa inahusika na utangazaji kwa
bidhaa mbalimbali, lakini pia inajihusisha na uibuaji wa vipaji kwa
vijana na watoto hususan wa vijiji kwa lengo la kuwajengea uwezo na
kutambua kuwa vipaji vingi vinaweza kutumiwa kama ajira.

Post a Comment