ad

ad

SUNZU AFUKUZWA MAZOEZINI SIMBA, AJIUNGA BONGO MUVI.

Felix Sunzu akifanya mazoezi na wachezaji wa Bongo Muvi baada ya kufukuzwa na kocha wake Patrick Liewig.
(Picha na Musa Mateja /GPL)


Na Wilbert Molandi
KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Liewig, juzi alimtimua straika wake wa kimataifa, Felix Sunzu katika mazoezi yake yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
 
Tukio hilo la kushangaza liliwaacha midomo wazi baadhi ya mashabiki wachache waliojitokeza uwanjani hapo, ambapo baada ya kufukuzwa, Sunzu alisogea kwenye uwanja wa pembeni na kujiunga katika mazoezi ya wachezaji wa Bongo Muvi yaliyokuwa yakiendelea muda huo.
 
Tukio hilo limetokea ikiwa ni muendelezo wa adhabu ya baadhi ya wachezaji wakongwe klabuni hapo kusimamishwa, chanzo kikiwa ni utovu wa nidhamu, baadhi yao ni Haruna Moshi ‘Boban’, Komambil Keita, Mwinyi Kazimoto, Ramadhani Chombo ‘Redondo’ na Amir Maftah.
 
Sunzu alifika mazoezini hapo akiwa na jezi za timu hiyo kwa ajili ya kuungana na wenzake, lakini dakika chache baadaye, mshambuliaji huyo aliitwa na Liewig na kutakiwa kuondoka kwenye mazoezi yaliyosimamiwa na msaidizi wake (Liewig) Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na Meneja, Moses Basena.
 
 Sunzu akifuata programu ya mazoezi ya wachezaji hao wa Bongo Muvi kwa umakini ikiwemo kukimbia mbio fupi na ndefu.
Taarifa za ndani zilieleza kuwa Kamati ya Utendaji ya timu hiyo ndiyo ilimruhusu Sunzu ajiunge na wenzake lakini kocha hakupewa taarifa.
 
“Kilichotokea katika mazoezi hayo, ni matatizo ya mawasiliano kati ya Kamati ya Utendaji na kocha ambayo yalichelewa kumfikia kabla ya kumfukuza mazoezini Sunzu,” kilisema chanzo.
Wakati huohuo, wakati tukienda mitamboni ilielezwa kuwa, Sunzu, Abdallah Juma na Kazimoto wanaweza kusamehewa, ambapo wametakiwa kuandika barua za kujieleza kisha warejeshwe kwa ajili ya mechi ya Yanga.
Powered by Blogger.