Sensa ya wafanyakazi wa serikali yafanyika nchini DRC baada ya miaka 30.
Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 30 serikali ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Kongo imefahamu idadi ya wafanyakazi wa idara za umma
nchini humo.
Kampeni ya sensa ya wafanyakazi wa serikali iliodhaminiwa na Afrika ya
kusini imemalizika nchini humo. Serikali ya Kongo imeelezea kwamba
ilikuwa ikipoteza kila mara dola milioni 20 kwa kuwalipa wafanyakazi
hewa, baada ya kubadili mfumo wa malipo ambao hivi sasa unafanyika
kupitia benki. Kwa sasa jumla ya wafanyakazi ni laki tatu na hamsini
elfu, zaidi ya nusu miongoni mwao wakiwa wazee. Mwandishi wetu Saleh
Mwanamilongo na ripoti kamili. Kuskiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya
spika za masikioni hapo chini.
Post a Comment