Rage atoa masharti matano kujiuzulu Simba.
LASTECK ALFRED
MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage amesema ana sababu nzito tano zitakazomfanya ajiuzulu wadhifa wake kama mwenyekiti wa Simba iwapo wanachama watathibitisha amefeli.
Rage amewasisitiza wanaomtuhumu kuwa ameshindwa uongozi wapime sababu hizo na wampinge kwa hoja thabiti. Kiongozi huyo aliliambia Mwanaspoti kuwa sababu ya kwanza ni wanachama wampime kama ni kosa kuongeza mapato ya klabu kupitia udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Alisema alipoingia Simba mwaka 2010, alikuta Simba ikipata udhamini wa Shilingi 192 milioni (kulingana na ripoti ya fedha ya Mkutano wa Simba wa Mwaka 2010 kabla ya kuingia madarakani), lakini sasa udhamini wa Simba (kwa ripoti ya mwaka 2012 unafika Shilingi 300 milioni pamoja na vifaa vya thamani ya Shilingi 70 milioni kwa mwaka.
Pili, alisema anaweza kujiuzulu kama kuongeza bei ya pango la biashara kwenye majengo ya klabu yaliyopo Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam ni kosa.
Zaidi ya miaka 15 iliyopita, klabu ya Simba ilikuwa ikipangisha pango kwa Sh. 200,000, lakini tangu nimeingia madarakani pango limepanda mpaka Sh. 1,500,000 kwa mwezi, yeyote anayepinga na hayo basi awasilishe hilo siku ya Mkutano Mkuu na nitajiuzulu, alieleza Rage.
Rage pia aliitaja hoja nyingine kuwa ni kufanya kwake marekebisho kwa Jengo la Simba lililopo Msimbazi ambalo kwa zaidi ya miaka 15 lilikuwa chakavu na halivutii.
Kingine cha nne anachoeleza katibu huyo wa zamani wa Simba ni kama kukodi na kuruhusu hoteli ndogo kujengwa katika eneo la Simba katikati ya jengo la zamani na jipya ni kosa. Hoteli hiyo inailipa Simba kodi ya Shilingi milioni 36 kwa kila mwaka.
Kumuuza Emmanuel Okwi kutoka Simba kwenda katika klabu ya Etoile Sportive Du Sahel ya Tunisia kwa ada ya dola za Kimarekani 300,000 ambazo bila hivyo Simba isingepata hata shilingi moja na Okwi angeondoka kama mchezaji huru.
Rage alisema alimuwahi mchezaji huyo na kumsainisha na ndio maana wakamuuza fedha nyingi.
Rage ameeleza kuwa kama hayo ndiyo makosa basi wanachama wamthibitishie na ajiuzulu kwenye mkutano halali.

Via Mwanasport.

Post a Comment