Diamond na Ney wa Mitego, hali halisi ya wasanii wa Tanzania.
Wimbo wa ‘Muziki Gani’ ilioimbwa na wakali wa muziki wa kizazi
kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Emmanuel Elibariki ‘Ney wa
Mitego’ umenifanya nikumbuke mikasa, visa wanavyofanyiana baadhi ya
wasanii nchini ambao hujigawa katika makundi mawili ya ‘wabana pua’ na
wale wanaoimba Hiphop.
Licha ya wimbo huo kutamba kwa muda mfupi, huku ukipigwa kila uchwao katika vituo mbalimbali vya redio, mashairi yake yanafafanua ukweli halisi kati ya makundi hayo mawili.
Hata hivyo, pamoja na hayo ukweli unabaki palepale kwamba matatizo yanayowakabili wasanii nchini ni yaleyale.
Tungo za wimbo huo zinafikisha ujumbe mahusus kwa wasanii kwamba wakati wa kupigana vikumbo umekwisha, sasa ni muda wa kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano wa hali ya juu bila kujali huyu anaimba, yule anarap.
Kipindi cha sanaa kuwa ridhaa na burudani kimepita, sasa ni wakati wa wasanii wenyewe kupigana kuhakikisha tasnia hiyo inakuwa chanzo cha kuwazalishia kipato.
Nikianza katika vyanzo vya mapato, msanii yeyote hata yule anayetoka kwenye mataifa yaliyoendelea vyanzo vyake vya mapato vinategemea zaidi mauzo ya kazi zake.
Mbali na hilo ipo mikataba anayosaini kushiriki matamasha na matangazo mbalimbali ya biashara.
Ni jambo lililowazi kuwa vyanzo hivyo vya mapato
vinategemea zaidi mfumo mzima wa usambazaji, katika hili msanii binafsi
ndiyo anatakiwa kuwa kidete kuhakikisha hakuna ujanja unaofanyika na
watu wengine wenye lengo la kumdhurumu mapato yake.
Kwa maneno mengine pamoja na ukweli kuwa, wasanii wanalazimika kuwekeza fedha wanazozipata kama wanavyofanya wasanii wa nje ili kutanua wigo wa vyanzo vya mapato, bado kwa hapa kwetu hali ni tofauti.
Wapo ambao hawaichukulii sanaa kama biashara, hata kile kidogo wanachokipata wanakitumia katika masuala yasiyo ya uzalishaji.
Ni wasanii wachache nchini ambao wanatajwa kuwa na vitega uchumi, kutumia umaarufu wao kujipatia fedha katika nyanja mbalimbali.
Huu siyo muda wa wasanii kubweteka baada ya kupata
umaarufu, bali ni muda wa wa kukwepa skendo, kuacha kushinda baa na
kujipanga kuutumia umaarufu katika kutanua vyanzo vingine vya mapato.
Nguzo kuu ni kuwa na umoja usiotetereka na usiobeba maslahi ya mtu yeyote ili kuwaondoa walioingia katika tasnia hiyo kwa lengo la kutumia migongo ya wasanii kujipatia fedha.
Naamini kabisa umoja wenye nguvu utakaosimamiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) utawafanya wasanii kuwa na sauti ya pamoja katika kila jambo linalogusa kazi zao.
Kwa ushirikiano wasanii wataweza kuwa na msimamo mmoja kuhakikisha hawashiriki tukio lolote bila kuhakikishiwa malipo yanayokidhi na ambayo yameandikwa katika mikataba husika.
Ni lazima ifike mahali wasanii waelewe kuwa, maisha si umaarufu
tu, kupata umaarufu ni jambo moja, tena lisilo na maana kama fedha
mfukoni hakuna.
Kikubwa ambacho kitawakomboa wasanii ni kutetea
masilahi yao bila kujali tofauti zao kwani bila wao kuonyesha mfano,
wasitegemee kama kuna mtu ataibuka na kuwasaidia katika hilo.
Nguzo kuu ni kuwa na umoja usiotetereka na usiobeba maslahi ya mtu yeyote ili kuwaondoa walioingia katika tasnia hiyo kwa lengo la kutumia migongo ya wasanii kujipatia fedha.
Kama wasanii wataendelea kuwa katika utengano kama
ilivyo sasa, sidhani kama wataweza kuwa na sauti dhidi ya wanaowahujumu
katika kazi zao.
Naamini kabisa umoja wenye nguvu utakaosimamiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) utawafanya wasanii kuwa na sauti ya pamoja katika kila jambo linalogusa kazi zao.
Mfano mzuri ni jinsi nyimbo za wasanii hao
zinavyotumiwa na kampuni mbalimbali za simu ambazo zinaingiza mamilioni
huku wasanii wakiambulia Sh500,000.
Ingawa ni vigumu kuwa na bei moja ya kazi zao au
malipo sawa kwenye maonesho, matamasha kutokana na soko huria, lakini
wasanii wakiwa na umoja wenye nguvu wanaweza kabisa kuwa na nguvu moja
ya kutetea maslahi yao.
Kwa ushirikiano wasanii wataweza kuwa na msimamo mmoja kuhakikisha hawashiriki tukio lolote bila kuhakikishiwa malipo yanayokidhi na ambayo yameandikwa katika mikataba husika.
Wasanii wakifika mahali wakawa na umoja hasa kwa
kuzingatia nguvu na nafasi waliyonayo katika jamii, wanaweza kukataa
kila aina ya dhuluma, unyonyaji na malipo duni kwenye maonesho na
matamasha.
Heko Diamond na Ney wa Mitego kwa kueleza kisa cha
kweli ambacho binafsi naamini kipo na ndiyo kinachochangia kuwafanya
wasanii waishi kwa makundi.
Mashabiki wenu ni wale wale, studio mnazorekodi
nyimbo zenu ni zilezile, kuweni kitu kimoja kwa maslahi yenu na taiofa
kwa ujumla.
Fidelis Butahe ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi.
Post a Comment