ad

ad

Jaydee kuadhimisha miaka 10 katika fani.

MSANII nguli asiyechuja katika nyimbo zake, Judith Wambura, ‘Lady Jaydee’ amewashukuru wadau na mashabiki wake kwa kuendelea kumuunga mkono na kumpa nguvu.

Akizungumzia sherehe za kutimiza miaka 13 tangu aanze kazi ya muziki, Jaydee alisema kuwa ameandaa sherehe kabambe itakayoambatana na uzinduzi wa albamu yake ya sita ‘Nothing But The Truth’.

“Kwa mwaka huu wa 2013, natimiza miaka 13 toka nianze kazi ya muziki, namshukuru Mungu, umma wa Tanzania kwa kuendelea kusapoti muziki wa Tanzania na kunipa nguvu mimi kama msanii, hivyo napenda wajumuike nami na kuendelea kuniunga mkono,” alisema.

Jaydee alisema kuwa uzinduzi wa albamu hiyo, unadhaminiwa na runinga ya East Africa (EATV), ambapo atawaburudisha mashabiki wake kwa kuimba nyimbo zake ambazo zilibamba miaka ya nyuma.

Uzinduzi na sherehe hizo utafanyika Mei 31, mwaka huu na kuwataka wapenzi na mashabiki wake kujitokeza na kumuunga mkono.
Powered by Blogger.