Roma, Madee, Nay wa Mitego wafunika Airtel Yatosha Mwanza.
WASANII wa muziki wa kizazi kipya ‘Bongo Fleva’ wamefunika kwa
kutoa burudani ya nguvu kwenye kampeni ya ‘Airtel Yatosha’ kwa kuwapa
raha maelfu ya wapenzi wa muziki huo waliofurika kwenye viwanja vya wazi
vya Furahisha jijini Mwanza.
Kampeni hiyo ya siku mbili inayoendeshwa na Kampuni ya simu ya
Airtel iliyofanyika katika viwanja hivyo, maelfu ya wananchi wa Mkoa wa
Mwanza walipata ushuhuda wa Airtel
Yatosha kwa kununua laini
za simu za mkononi za kampuni hiyo na jinsi ya kutumia huduma ya
internet, kuongea kwa kujiunga na kupata dakika nyingi za muda wa
maongezi kwenda mitandao mingine kwa bei nafuu zaidi kwa laini moja tu
ya Airtel.
Wasanii wa Bongo Fleva waliotoa burudani na kuwaacha hoi
maelfu ya wananchi waliofurika kupitia vibao vyao vinavyotamba kwenye
vituo mbalimbali vya redio na runinga hapa nchini ni pamoja na Juma
Kassim ‘Sir Nature’ na kundi lake la Wanaume Halisi, Roma Mkatoliki,
Madee na Ney wa Mitego.
Maelfu ya wananchi walioshuhudia kampeni hiyo waliweza pia
kushuhudia vipaji vya uimbaji kutoka kwa vijana walioshindanishwa na
waliojitokeza kucheza muziki wa Bongo fleva katika viwanja hivyo na
kupata zawadi za laini na fulana za Airtel.
“Wananchi wengi wamekuja hapa kupata burudani kutoka kwa
wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongo fleva kama ulivyojionea, lakini
pia wengi kwa sasa wanatumia mtandao wa Airtel, ikiwamo huduma hii ya
Airtel Yatosha pamoja na kununua laini na kupatiwa maelezo ya jinsi ya
kutumia huduma hii,” alisema msanii Ney wa Mitego.
Akizungumzia kampeni hiyo, Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo,
Jackson Mmbando alisema kwamba tangu kuzinduliwa na kufanyika katika
mikoa sita hadi sasa hapa nchini, kumekuwa na mapokeo na mafanikio
makubwa kwa kuongeza wateja wanaotumia mtandao wa Airtel kupitia huduma
zote.
Mfanyabiashara wa vituo vya kuuza mafuta, Barnabas Mathayo wa
jijini Mwanza, alitoa ushuhuda wa kukubali huduma inayotolewa na Airtel
katika mahojiano maalumu, akisema kwamba tangu kuanzishwa kampeni ya
Airtel Yatosha, amekuwa akinunua kifurushi na kujiunga na kujipatia muda
wa kutosha kufanya mawasiliano na ndugu, rafiki, wavuvi wanaonunua
mafuta kwa ajli ya boti zao pamoja na wafanyabiashara mbalimbali kupitia
mitandao yote kwa bei ile ile.
Kampeni hiyo inaendelea katika mikoa mingine na mwishoni mwa
juma hili itahamia jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Zakhem.


Post a Comment