HANS POPPE AREJEA MADARAKANI SIMBA SC
SASA
ni shwari Simba SC. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema, kufuatia pande
mbili zilizokuwa zinavutana, uongozi chini ya Mwenyekiti Alhaj Ismail
Aden Rage na wapinzani wake kumaliza tofauti zao.
Pongezi
kubwa ziende kwake, Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ), Zacharia Hans Poppe aliyefanikisha kumaliza mgogoro wa chini kwa
chini baina ya Rage na wapinzani wake.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jioni hii, mpatanishi huyo wa mgogoro uliorejesha amani na umoja Simba SC, amesema; “Tofauti zilizokuwapo tumekwishazimaliza na sasa Simba SC ni shwari, tunaanza upya kazi,”alisema.

Poppe
aliyepigana vita dhidi ya Nduli Iddi Amin Dada kuokoa ardhi ya Tanzania
na Watanzania waliokuwa wakinyanyswa na askari na rais huyo wa zamani
wa Uganda, aliongeza; “Na kwa maana hiyo, natamka rasmi, nami nimerejea
ndani ya Simba SC kwa nafasi zangu zote kama nilivyoombwa baada ya
kujiuzulu,”alisema.
Poppe
alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili- wakati huo huo Mwenyekiti wa Friends Of Simba na aliamua kukaa
kando kabisa wakati mgogoro kutofungana na upande wowote, akishughulikia
amani ya klabu.
Poppe
alisema kwa sasa wanalekeza nguvu zao katika kumalizia Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara kwa heshima na baada ya hapo watatengeneza timu
mpya itakayoiteka soka ya nchi hii msimu ujao.
“Tumevuna matunda ya ugomvi na migogoro katika klabu, tulianza msimu vizuri na tukawa juu kwa muda mrefu, lakini baada ya hapo naona tukalewa mafanikio tukaanza kugombana bila sababu,”.
“Tumevuna matunda ya ugomvi na migogoro katika klabu, tulianza msimu vizuri na tukawa juu kwa muda mrefu, lakini baada ya hapo naona tukalewa mafanikio tukaanza kugombana bila sababu,”.
“Matokeo
yake ndiyo haya, tumepoteza mwelekeo, lakini madhali tumemaliza tofauti
baina yetu, na tumefikia makubaliano ya msingi ya kudumisha umoja na
amani ndani ya klabu, ambavyo ndivyo chimbuko la mafanikio, hakuna shaka
wana Simba watafurahi tena,”alisema Hans Poppe.
Mambo yalitibuka Simba SC miezi kadhaa iliyopita kufuatia mgogoro wa chini kwa chini baina ya Rage na wapinzani wake, uliosababisha mgawanyiko hadi ndani ya uongozi.
Mambo yalitibuka Simba SC miezi kadhaa iliyopita kufuatia mgogoro wa chini kwa chini baina ya Rage na wapinzani wake, uliosababisha mgawanyiko hadi ndani ya uongozi.
Makamu
Mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ alijiuzulu sambamba na Hans Poppe
na tangu hapo, Simba imekuwa ikienda kama jahazi liso na Nahodha na
matokeo yake ni kutaka kuzama kwa kupoteza mwelekeo.
Matokeo yake, timu imepoteza ubingwa wa Ligi Kuu na kukosa hata nafasi ya pili, ambayo ingewawezesha kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
Amani inarejea Simba SC zikiwa zimebaki takriban wiki tatu kabla ya kumenyana na wapinzani wa jadi, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga SC walitaka sana kutumia mwanya wa mgogoro ndani ya Simba SC kulipa kisasi cha kufungwa 5-0 mwaka jana, lakini sasa inaonekana shughuli itakuwa pevu Mei 18 Uwanja wa Taifa.

Post a Comment