ad

ad

Arsenal kuivaa West Brom leo

London, England. 
Arsenal leo inarejea kwenye uwanja uliocheza na kupata ushindi uliowapa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa siku ya mwisho ya kumalizika kwa Ligi Kuu England msimu uliopita wakisaka ushindi mbele ya West Brom watakaokuwa uwanja wa nyumbani.


Pia kutakuwa na michezo mingine, ambapo Reading itakuwa nyumbani kucheza na Southampton, kadhalika Norwich wataisubiri nyumbani Swansea, huku Aston Villa wakiwa wageni wa Stoke City.

Zikiwa mechi nane zimesalia kabla ya kumalizika msimu, Kocha Arsene Wenger hajakata tamaa kwamba kikosi chake hakina nafasi miongoni mwa nne za juu.
Gunners wameshinda mechi tano kati ya sita za mwisho za Ligi Kuu na kuvuna pointi 19, lakini ikiwa nyuma kwa pointi 24 dhidi ya wanaoongoza ligi, Manchester United.
Ni mchezo mmoja tu waliopoteza dhidi ya majirani zao Tottenham, lakini kiwango kizuri walichoonyesha Munich kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa, kimewatia nguvu kwenye mechi za ligi ya nyumbani.

Kiwango walichoonyesha katika mchezo wa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Swansea kilikuwa kielelezo kizuri cha kuonyesha dhamira ya kusaka moja ya nafasi nne za juu kwenye msimamo.
Katika mchezo wa leo, Arsenal inaweza kuwa dimbani na wachezaji Jack Wilshere na Theo Walcott.
Kocha Msaidizi, Steve Bould amebainisha ni mapema kusema lolote kuhusu uwezekano wa wachezaji hao kuanza kwenye kikosi cha kwanza leo.
Youssouf Mulumbu ataukosa mchezo wa leo kutokana na kuanza kutumikia kadi nyekundu dhidi yan West Ham wiki jana.
Powered by Blogger.