Wambura atupwa Uchaguzi TFF
BAADA ya kuvuka kikwazo cha pingamizi katika jaribio la kurejea
kuongoza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura ameenguliwa
kugombea uchaguzi wa shirikisho hilo.
Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho hilo unatarajiwa
kufanyika baadaye mwezi huu, ambapo Wambura aliomba kuwania nafasi ya
makamu wa rais.

Akiongea na gazeti hili jana, Wambura alisema mpaka jioni ya jana hakuwa na taarifa za kuenguliwa kwake kwenye uchaguzi huo.“Sina taarifa za jina langu kutopita kwenye usaili, kama ni kweli, nafahamu kuwa sababu ni zilezile.
Nitaangalia kama sababu ya kutaka rufaa itakuwapo,” alisema Wambura.
Mara ya mwisho Wambura, Katibu Mkuu wa kilichokuwa Chama cha Soka Tanzania (FAT) kushiriki uchaguzi wa shirikisho hilo ilikuwa mwaka 2004 alipoangushwa na Leodegar Tenga, rais anayemaliza muda wake.
Wambura amekuwa akienguliwa mara kwa mara katika chaguzi za vyama vya soka, ambapo aliwahi kutupwa ne kwenye uchaguzi wa Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) Pia jina lake liliondolewa kwenye uchaguzi wa Chama cha Soka Mara, pia hakushiriki kwenye Uchaguzi wa TFF mwaka 2008.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Deogratius Lyato alisema kuwa Wambura ameenguliwa kwenye kinyang’anyiro hicho kwa vile hajakidhi matakwa ya uchaguzi ibara ya 9 (7) Ibara hiyo inaeleza kuwa na uadilifu wa kusimamia na na uwezo wa kufanya kazi kikamilifu, kutimiza wajibu na malengo ya TFF.
Katika ufafanuzi wake, Lyatto alisema pia Wambura alizivunja Katiba ya Klabu ya Simba Ibara 11 (2) (b), Katiba ya TFF Ibara 12 (1) (d) na 12 (2) (e), na Katiba ya Fifa Ibara ya 64 (2) mwaka 2010, alipompeleka Mwenyekiti wa Simba mahakamani kinyume na Katiba za vyama vyote hapo juu.
Hata hivyo kwa mujibu wa Katiba ya TFF Ibara ya 49 (1), na Kanuni za Uchaguzi za Mwanachama wa TFF Ibara ya 26 (2), Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kutumia mamlaka yake kikatiba na kanuni za uchaguzi ilimuhoji Wambura kuhusu taarifa za kufungua kesi namba 100 mwaka 2010, Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu dhidi ya Mwenyekiti wa Simba (Hassan Dalali) na hivyo kwenda kinyume na Katiba ya Simba, TFF, CAF na Fifa ambayo inazuia masuala ya soka kupeleka mahakamani.
“Kamati inaheshimu uamuzi uliotolewa na Kamati ya Rufaa ya TFF kuhusu uchaguzi mwaka 2008, kwamba Wambura hakukidhi matakwa ya Ibara ya 29(7) ya Katiba ya TFF na Ibara ya 9 ya Kanuni za Uchaguzi za TFF.
“Kwa mujibu wa Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF haina mamlaka ya kubadilisha uamuzi uliofikiwa na Kamati ya Rufaa.
Uamuzi huo unaweza tu kubadilishwa na Mahakama ya usuluhishi wa masuala ya michezo (CAS),” alisisitiza Lyato.
Wambura ambaye alipangua mapingamizi yaliyowekwa dhidi yake na mwanachama wa Simba Said Rubeya amekuwa mbali na Wambura, pia Mwenyekiti wa Azam, Mohamed Said anakalia kuti kavu kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bodi kwa kuwa kupitishwa kwake kutategemea matokeo ya uhakiki wa vyeti vyake.
Mbali Wambura wengine walioenguliwa kwenye kinyang’anyiro hicho ni Eliud Mvela aliyekuwa akitetea nafasi yake ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF kupitia Mkoa wa Iringa na Mbeya.
Lyato alisema kuwa Mvela ameenguliwa kwa vile hajakidhi matakwa kwa kukiuka kanuni ya 9 ibara ya (7) na kwamba siyo mwaminifu kwa kuwa alishiriki uamuzi Kamati ya Utendaji ya kufanya mabadiliko ya katiba lakini matokeo yake aliigeuka na kuipinga.
“Mvela alitakiwa ile siku kamati ya utendaji imekaa angejiorodhesha kutounga mkono suala hilo lakini alishiriki mchakato mpaka mwisho, dakika za mwisho katika utekelezaji aliigeuka kamati,” alisema Lyato.
Post a Comment