ad

ad

MAJANGA BRAZIL: KLABU YA USIKU YAWAKA MOTO, WATU 245 WAPOTEZA MAISHA

KARIBU watu 245 wamekufa katika klabu ya usiku nchini Brazil baada ya kushika moto alfajiri ya Jumapili wakati bendi ikitumbuiza.
Taarifa za awali zimesema kuwa watu 90 wameteketea kabisa, lakini idadi ya vifo imezidi kuongezeka kadiri maiti zinapoibuliwa katika klabu hiyo ya Kiss iliyopo katika mji wa Santa Maria, kwenye Jimbo la Rio Grande do Sul.


Wakati maofisa wakisema sababu ya moto bado kujulikana, taarifa zinadai kuwa chanzo ni miale ya moto iliyokuwa ikiwashwa kwa furaha na watu waliofurika ukumbuni humo wakati bendi ikitumbuiza.
Polisi wa kiraia na msemaji wa serikali katika ukanda huo, Marcelo Arigoni aliiambia Radio Gaucha kwamba idadi kamili ya wahanga bado haijajulikana, lakini mamia ya watu wanaelezwa kujeruhiwa – karibu watu 200.
Aliiambia redio hiyo kuwa lori lililobeba miili 70 liliwasili katika kituo cha michezo cha Manispaa kilichotengwa kwa ajili ya kukusanya miili hiyo.
Polisi wanaamini kuna karibu miili 20 ndani ya klabu hiyo.
Mmoja wa walinzi wa klabu hiyo, Rodrigo Moura, alikaririwa akisema kuwa kulikuwa na watu kati ya 1,000 na 2,000.
Rais wa Brazil, Bi. Dilma Rousseff amelazimika kufuta ushiriki wake katika mkutano wa kikanda nchibni Chile na kurudi nyumbani haraka kufutia habari za janga hilo.
Via saliti 5
Powered by Blogger.