Aliyepigwa Risasi na Polisi na Kufariki Wakati wa Maandamano ya CHADEMA Ni Mwanafunzi wa NIT, Sio UDSM
Serikali
ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) imepokea kwa
mshituko taarifa za kifo cha mwanafunzi Aqulina Akwilini ambaye
inasemekana amepigwa risasi na polisi wakati wakikabiliana na
waandamanaji wa Chadema jana.
Awali
taarifa hizo zilimhusisha mwanafunzi huyo na Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM) lakini baada ya uchunguzi wa kina imebainika ni mwanafunzi
anayesoma Chuo cha Usafirishaji (NIT) mwaka wa kwanza.
Daruso
inalaani vikali kitendo hicho kilichotokea na kutumia nafasi hii
kushauri polisi kujitafakari kama ni sahihi kupambana na raia wa
Tanzania kwa kutumia silaha za moto.
Daruso
pia amekitaja kitendo hicho kuwa ni cha kinyama na cha kulaaniwa na
kukemewa na kila Mtanzania yeyote bila kujali tofauti za kisiasa.
‘’Pamoja
na tofauti zetu nyingi kama vyama , dini ,ukabila na kadhalika , taifa
letu limejengwa kwenye misingi ya undugu, umoja, mshikamano na si
matumizi ya nguvu kupita kiasi au kukiuka sheria na taratibu za nchi
yetu,’’ imesema barua hiyo ya Daruso kwa vyombo vya habari.
Post a Comment