Uchaguzi Kinondoni: Mkurugenzi Afafanua Mawakala Kuzuiwa Kuingia
Wakati
baadhi ya vituo vya kupigia kura katika uchaguzi wa jimbo la Kinondoni
mawakala wa vyama vya siasa wamezuiwa kuingia kwa madai kuwa barua zao
za viapo zimekosewa, msimamizi wa uchaguzi huo, Aron Kagurumjuli amesema
uchaguzi huo unakwenda vizuri.
Baadhi
ya mawakala hao katika kituo cha Lasko kilichopo kata ya Tandale
wamezuiwa kwa madai kuwa hati zao za uthibitisho walizopewa zimekosewa.
Akizungumza
leo Februari 17, 2018 msimamizi wa mawakala wa CUF kata ya Tandale,
Abdul Zain amesema wamefika vituoni tangu saa 12 asubuhi lakini mawakala
wao wamezuiwa kuingia ndani ya vituo hadi hati zao zitakapobadilishwa.
Amesema kuwa wamefuatilia suala hilo ofisi za Kagurumjuli na kupewa fomu nyingine ambazo pia zimekataliwa.
Katika
ufafanuzi wake, Kagurumjuli amesema mawakala wengi hawakuwa na barua
kutoka NEC zinazowatambulisha kuwa ni mawakala ambazo walitakiwa kupewa
na viongozi wa vyama vyao na badala yake wanatumia barua za viapo
alizodai kisheria haziwezi kuwa utambulisho pekee wa kuwa mawakala.
Amefafanua kuwa barua hizo za viapo hazitumiki kuwahalalisha, kwamba vituo vyote katika kata tano wameshatatua tatizo hilo.
“Wakala
anapaswa kuapa kwanza na barua ya kiapo napaswa kuwa nayo mimi ili
wakifanya kosa niwachukulie hatua. Kiapo si mali yao ndiyo maana
tuliwapa nakala, hakuna sheria ya kupewa barua ya kiapo kuna sheria
inayosema wakala ataapa siku saba kabla ya uchaguzi na ndivyo
ilivyofanyika,” amesema.
“Barua
ya utambulisho ndiyo kitu muhimu wanapaswa kuwa nazo ambazo zimetolewa
na ofisi ya Mkurugenzi. Barua ya kiapo siyo suluhisho la kuingia nayo
kwenye kituo ila barua ya utambulisho ndiyo inahusika.”
Kuhusu
matokeo kutangazwa amesema, “Tunatarajia hadi saa sita usiku matokeo
yatakuwa yameshajulikana iwapo kura zitapigwa vizuri na kuhesabiwa bila
vurugu.”
Post a Comment