ad

ad

NIT Yakiri Aliyepigwa risasi na polisi ni mwanafunzi wao


Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) kimesema aliyepigwa risasi jana Februari 16, 2018 eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam na kufariki dunia ni mwanafunzi wa chuo hicho.

Chuo hicho kimemtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Akwilina Akwiline aliyekuwa anasoma shahada ya kwanza ya ununuzi na ugavi.

Leo, Februari 17, 2018, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekiri mtu mmoja kupigwa risasi na polisi wakati wakiwatawanya wafuasi wa Chadema walioandamana jana.

Wafuasi hao wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe waliandamana kuelelea ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni, Aron Kagurumjuli kudai viapo vya mawakala wa chama hicho.

Ofisa Uhusiano wa NIT, Ngasekela David amesema wamepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha wanafunzi huyo.

"Ni kweli alikuwa wanafunzi wetu na tumepokea kwa masikitiko taarifa hizi. Tunaendelea kufuatilia zaidi, "amesema David.

No comments

Powered by Blogger.