Wema Sepetu afunguka kwa mara ya kwanza tangu atoke mahabusu
Msanii
wa filamu nchini Wema Sepetu leo amefunguka na kuwashukuru mashabiki
wake kwa kumpa faraja na kumuombea katika kipindi chote ambacho alikuwa
matatizoni
"Mimi
na familia yangu tunapenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zetu za
dhati kwa wote mlioshirikiana nasi kwa hali na mali katika kipindi hiki
kigumu tulichopitia. Najua wengi mlikua mnaniombea, nashukuru kwa sala
na dua zenu kwani zimenisaidia kwa kunipa nguvu wakati nikiwa kwenye
wakati mgumu sana kwenye maisha yangu". Aliandika Wema Sepetu
Wema
aliendelea kutoa shukrani zake kwa wasanii pomoja na mwanasheria wake
ambao walikuwa naye katika kipindi hicho kigumu katika maisha yake.
"Napenda
kuwashukuru mashabiki wangu wote duniani kwa kuniamini na kusimama na
mimi kwa kipindi chote hiki, pia napenda kuwashukuru wasanii wenzangu
wote. Asante sana kwa mwanasheria wangu Alberto Msando kwa kunisimamia
na kuwa na mimi bega kwa bega wakati huu mgumu. Nakuombea kwa Mungu
akupe moyo huohuo wa kuwatetea wanyonge". Aliandika Wema Sepetu
Post a Comment