ad

ad

Wema, Tunda, Mobeto Wanavyozungukana!

Wema.

DAR ES SALAAM: Mambo ni moto! Habari ya mjini inayotrendi ni kitendo cha staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu kuonekana akioneshana mahaba shatashata na zilipendwa wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambacho kimeamsha ‘vilivyolala’.
Wema na Diamond ‘walifanya yao’ wikiendi iliyopita kwenye ‘iventi’ ya Wasafi Classic Baby (WCB) kumsaini msanii mpya katika lebo yao, Mbwana Yusuf Kilungi ‘Marombosso au ‘Mbosso’ iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Nyota Tano ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro iliyopo Posta jijini Dar kisha kujiachia kwenda kwenye Klabu ya Maisha Basement, Kijitonyama, usiku huohuo.
Kufuatia tukio hilo, wakali wa ubuyu walilidokeza Risasi Mchanganyiko kuwa, kwa muda mrefu sasa kumekuwa na skendo ya mastaa wa kike, Wema, Video Queens, Tunda Sebastian na Hamisa Mobeto kudaiwa kuzungukana kwa jamaa huyo.
Chanzo makini kilimwaga ubuyu kuwa, kabla ya Mobeto kutangaza kubeba ujauzito wa Diamond kisha kujifungua mtoto wa kiume, Prince Dully kulikuwa na ‘unyunyuz’ kuwa, Wema alikuwa akionekana nyumbani kwa jamaa huyo, Madale-Tegeta, Dar.
Mobeto.

Hata hivyo, Wema na Diamond ambao walikuwa wapenzi wa kukata na shoka kabla ya kumwagana, walikanusha kwa nguvu zote kuwa hawakuwa wamerudiana.
Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kuwa, jambo hilo lilisababisha kuwepo kwa msuguano mkali kati ya Wema na mzazi mwenza wa Diamond, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
MOBETO
Msuguano huo ulimalizwa na skendo ya Diamond kuzaa na Mobeto ambapo sasa Zari na timu yake waliachana na Wema na kuhamishia mashambulizi kwa Mobeto.
Katika maelezo yake, Diamond alikiri kumsaliti Zari na kuzaa na Mobeto.
TUNDA
Ilisemekana kuwa, wakati mambo yakiwa ni moto kati ya Mobeto na Zari, ghafla upepo ulibadilika baada ya kuibuka kwa skendo mpya kuwa, Tunda naye anatoka na Diamond.
Tunda

Ilidaiwa kuwa, kwa nyakati tofauti, Tunda alionekana nyumbani kwa Diamond, Madale-Tegeta, Dar na kujiachia na jamaa huyo kwenye klabu mbalimbali za usiku ikiwepo Elements iliyopo Masaki, Dar.
“Kama hiyo haitoshi, mambo yalipamba moto zaidi baada ya kuwepo kwa ubuyu kuwa Tunda naye ana mimba ya Diamond,” kilidai chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina.
Alipobanwa na gazeti damu moja na hili, Ijumaa Wikienda juu ya kuwa na uhusiano na kubeba mimba ya Diamond, Tunda alidai kuwa jamaa huyo ni sawa na kaka yake, lakini akakiri kuwa na mimba.
WEMA
Katika tukio la wikiendi iliyopita, Wema alibanwa na Global TV Online juu ya uhusiano wake na Diamond ambapo alisema: “Utoto umekwisha, tunasapotiana na hatutaacha kufanya hivyo. Najua watu wanasema kwa sababu ‘kapo’ yetu ilikuwa gumzo mno kwa mashabiki wetu.”
DIAMOND
Kwa upande wake Diamond, alipoulizwa juu ya uhusiano wake na Wema na kwamba ilikuwaje hadi akamwalika kwenye tukio hilo alisema:
“Mimi ndiye niliyempigia simu nikamuomba aje kwenye iventi yetu na amekuja, hakuna ubaya, amekuja kutusapoti, kunakuwa na mambo mengi kwa sababu tulikuwa wapenzi zamani, lakini kwa sasa tunapeana sapoti ya kazi zetu tu.”
Kuhusu Tunda na Mobeto, Diamond alisema: “Kuhusu Tunda…yupo hapa, niliwaalika wote, nimemuona yumo…oya Tunda hebu njoo (akapotezea).
“Hivi ina maana kila mtoto mzuri mimi nina…(akimaanisha anakuwa naye kimapenzi), si kweli…”
“Kuhusu Mobeto, kama nilivyosema, niliwaalika wote , lakini hajafika.”
KIFUATACHO…
Kufuatia kilichojiri kati ya Diamond na Wema kisha kusambaa kwa picha za video na mnato, wafuatiliaji wa mambo ya ubuyu wanadai kuwa, kwa vyovyote Wema atakuwa amemtibua upya Zari hivyo anatarajiwa kujibu mapigo muda wowote.
STORI: Mwandishi Wetu, Risasi Mchanganyiko

No comments

Powered by Blogger.