Mume Ampiga Stop Shamsa Mitandaoni
Shamsa Ford
Chanzo kilieleza kwamba Chid Mapenzi alimpiga marufuku mkewe Shamsa kutumia mitandao ya kijamii kwa kuwa muda mwingi alikuwa akiutumia kwenye mitandao hiyo huku wakati mwingine akiambulia matusi kutoka kwa mashabiki zake jambo ambalo lilimchefua mumewe huyo na kuamua kumkataza.
Alipoulizwa Shamsa kuhusiana na suala hilo alikiri kwamba ni kweli mumewe alimtaka atoke kwenye mitandao ya kijamii kwa muda mpaka atakapomruhusu tena na hajui sababu za kukatazwa.
“Kwa sasa naishi kwa amani sana maana nimepumzika na matusi ya mitandaoni siyaoni tena, sijui mume wangu aliona nini ila aliniambia nitoke mpaka atakaponiruhusu tena ndiyo nitarudi,” alisema Shamsa.
Post a Comment