ad

ad

Wasanii 20 Wakatwa Fiesta Dar + Audio

Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, amesema wamepunguza wasanii 20 ambao awali walipangwa kuwepo kwenye Tamasha la Tigo Fiesta linalotarajiwa kufanyika Jumamosi katika vya Viwanja Leaders Club.

Ruge ameyasema hayo leo katika kipindi cha Clouds360, ambapo amesema: ‘’Tulikaa kama kamati jana na tumeamua kuachana na suala la muda, tumeamua tukae kwenye muda tulioupanga sisi na kuhakikisha tuna ‘six hours’ za burudani ambazo zimepangwa na kupangika.”
Ruge alisema miongoni mwa wasanii walioondolewa kutokana na muda ni Lulu Diva,  ChinBeez, Bright, Mimi Mars, Zaiid na wengineo.

No comments

Powered by Blogger.