ad

ad

Zari Aibuka Na Dongo Jingine Kwa Diamond

Leo katika akaunti ya Instagram Zari amefunguka hasa baada ya kuposti katika Snapchat akionesha kupinga kuhusu madai ya Diamond kwamba yeye alikuwa anajua ishu hiyo.

Jana katika Snapchat yake aliweka posti mbili zilizojaa baadhi ya maandishi yakimuendea Diamond wakati bado akiwa katika mahojiano.


“Unajichezea mwenyewe, uongo unaongea kuhusu mimi kwamba nilikuwa najua kuhusu huyo mpenzi wako wa kando. Nakuomba ujaribu kupambana na hali yako na acha kuongea uongo. 


Mimi kukaa kimya haimaanishi kwamba ni mjinga. Kuwa makini na maneno yako,” alimaliza.

“Mimi ni mama wa watoto wako ndio sababu naheshimu na kukaa kimya, ila jaribu ku-google maana ya kumdhalilisha mtu, usinijaribu mimi,” aliongeza.


“Lakini ebu tuangalie hili katika namna chanya zaidi. Mtu anapoamua kukusaliti wewe, sio wewe bali ni wao na kwa kawaida huwa wanakuwa wamejichezea wenyewe na si wewe kama walivyofikiria .


“Haitakiwi kukata tamaa na wala usifikiri kwamba wewe una thamani sana kwa makosa ya mtu Fulani na wala usijilaumu. Lakini kila siku jiangalie ni namna gani utajiinua mwenyewe na kuzidi kusonga mbele... kwa maana hiyo pamoja na sherehe yangu ya kuzaliwa inayokaribia  ebu mambo hasi yote tuyaache nyuma na tufarahie maisha,” ameandika leo katika akaunti yake ya Instagram.

No comments

Powered by Blogger.