ad

ad

Irene Uwoya: Napenda mwanaume mwenye sura ya Kiume Kama Ndikumana

MWIGIZAJI maarufu wa kike wa filamu za Bongo anayeitingisha Bongo Movie ambae pia aliwahi kuolewa na mcheza soka kutoka Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Katauti’, mlimbwende Irene Uwoya, amesema kuwa mpenzi wake wa sasa ana ngeu nyingi mwilini mwake kutokana na kuchanwa visu.
Uwoya amesema watu kama hao ndiyo anaowataka yeye, kwa sababu inaonyesha uanaume halisi, na si wanaume kuwa laini kama mtoto wa kike.


Alipoulizwa juu ya hilo alifunguka: “Sijasema napenda wanaume wenye sura mbaya. Nimesema napenda mwanaume mwenye sura ya kiume, mwanaume uwe na ngeu. Mimi bwana’angu ana ngeu za kuchanwa visu, viwembe na nahisi hata bunduki zimemkosakosa,” alisema Irene Uwoya
Mwigizaji huyo kwa sasa hajaweka wazi mahusiano yake tangu alipoachana na aliyekuwa mpenzi wake, msanii wa Bongo Fleva, Msami Baby, na amesema hataweka tena mahusiano yake wazi.

No comments

Powered by Blogger.