ad

ad

Kocha wa Azam Afunguka Mazito ndani Ya Timu Yake


 BAADA ya kikosi chake kuwa na matokeo mazuri ndani ya michezo mitatu waliyocheza hadi sasa, Kocha Mkuu wa Azam, Aristica Cioaba raia wa Romania amefunguka kwa kusema huo ni mwanzo lakini wataendelea kufanya makubwa kwa msimu huu ili kutimiza malengo waliyojiwekea ya kumaliza kwenye nafasi za juu ikiwezekana kutwaa ubingwa. 


Azam mpaka sasa haijapoteza mchezo wake wowote ule wa Ligi Kuu Bara baada ya kushuka dimbani mara tatu na kushinda mechi mbili dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara na Kagera Sugar huku wakitoka sare na Simba.
Kutokana na matokeo hayo, Azam ambayo haijafungwa hata bao moja imejikusanyia pointi saba ikiwa kwenye nafasi ya tatu. 


Akizungumza Mromania huyo amesema anafurahishwa na matokeo wanayoyapata lakini lengo lake ni kuona wanaendelea kushinda zaidi kwenye mechi zao kwa ajili ya kujikusanyia pointi ambazo zitawaweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi. 


“Huu ni mwanzo mzuri kwetu kwa kutopoteza hata mchezo mmoja, hii inaonyesha kwamba tulikuwa na muda mzuri wa kujiandaa kwa ajili ya hiki ambacho tunakionyesha leo mbele ya wapinzani wetu. 


“Lakini kwangu naona bado tuna kazi kubwa ya kufanya kwani ni lazima tuendeleze ubora wetu kwa kupata matokeo mazuri kwenye kila mchezo wetu ujao, na hilo tuna uhakika mkubwa wa kulitimiza kwa sababu tuna wachezaji bora ambao wapo tayari kwa ajili ya kupambania matokeo,” alisema kocha huyo.

No comments

Powered by Blogger.