Zullu Kurejea Uwanjani Soon, Daktari wa Yanga Athibitisha
Daktari wa Timu ya Young Africans, Edward Bavu, amewatoa hofu mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kuwa Hali ya Kiungo wa Kimataifa wa Zambia Justine Zullu si mbaya sana na anaweza kurejea katika michezo ya hivi karibuni.
Bavu amesema licha ya mchezaji huyo kuonekana kuumizwa sana na Kiungo wa Azam Fc Himid Mao Mkami, hali iliyopelekea kushonwa nyuzi tisa lakini jereha lake halijahusisha viungo hivyo anaweza kuwahi kurejea dimbani kuliko vile walivyotoa taarifa awali.
Ni jeraha dogo
-Unajua aliumia kwa kuchubuliwa Ngozi na si kuvunjwa mfupa, ingekuwa hivyo kupona kwake kungechukua muda kidogo lakini hivi anaweza kupona haraka, kwani ni jereha tu la kidonda likipona hili na maumivu kuisha basi atarajea mapema zaidi, tofauti na vile tulivyosema Mwanzoni’, amesema Bavu.
Awali taarifa ya klabu ilisema Zullu anaweza kukaa nje ya Dimba kwa zaidi ya siku 14 lakini sasa matumaini kwa Wanayanga yanaanza kurejea ukizingatia kwamba wao wanaongoza ligi kuu pamoja na Kushiriki michuano ya Shirikisho huku wengi wakimtaja Zullu kuwa msaada mkubwa katika Mashindano yote.
Kutokana na faulo hiyo, Kiungo wa Azam FC Himid Mao Mkami ameomba samahani na kumpa pole Justine Zullu huku akiongeza kuwa haikuwa nia yake kumuumiza bali ni bahati mbaya.
Post a Comment