ad

ad

Gwajima adai kutishiwa kifo na watu wasiojulikana


 Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema kuwa ametishiwa kifo na kundi la watu asiowafahamu.

Gwajima amesema hayo jana alipokuwa akihubiri katika kanisa lake lililopo Ubungo, Jijini Dar es Salaam.

Mchungaji huyo amedawa kuwa vitisho hivyo vilikuja kwa njia ya ujumbe ukimtahadharisha kuwa hatamaliza wiki inayoanza.

Gwajima ni miongoni mwa washukiwa waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.

No comments

Powered by Blogger.