Hope Lucy Ruhinda: Napenda Kuwa Na Mwanaume Asie Nipangia Aina Ya Mavazi Ya Kuvaa
Hope Lucy Ruhinda ( 25 ) ni mwanamitindo anae fanya vizuri sana katika tasnia ya urembo nchini Afrika.
Mwanamitindo
huyu ambaye ni mtanzania kwa mama, na mnyarwanda kwa baba,
kupitia kazi zake za mitindo , ameonyesha nia ya kufika mbali
katika tasnia ya mitindo., huku lengo lake likiwa kufikia
level za kimataifa kama Naomi Campbell.
Akielezea kuhus safari yake katika tasnia ya mitindo, Hope anasema
“Tangu
nikiwa shule ya msingi, siku zote nilikuwa nikitamani sana
kuwa muimbaji, dancer au mwanamitindo. Lakini kwa kuwa sikuwa na
kipaji cha kuimba wala kudance, nikaamua kujikita katika mitindo
“
Akaongeza“
Nilipofika O-Level nikaanza kufanya modeling for fun. Hapo
nilikuwa bado Tanzania. Nilipo maliza O-Level huko Tanzania,
nilikuja kujiunga na masomo ya A-Level katika shule ya
sekondari ya FAWE Girls’ Secondary School hapa Kigali.”
Nilipo
maliza A-Level nilienda kushiriki Miss Rwanda, baada ya
kushauriwa na kushawishiwa na rafiki zangu wa karibu. Mwanzoni
nilikuwa mgumu kukubali ushauri wao, lakini baada ya kutafakari
kwa muda, nikaamua kushiriki.
Kwenye
mashindano sikufanikiwa kuchukua taji la Miss Rwanda, Nililia
sana siku hiyo. Sababu kuu ya kushindwa kwangu, walitaka mtu
anaye weza kuzungumza Kinyarwanda fluent, na mimi sikuwa na
uwezo huo.
Hata
hivyo, shindano la Miss Rwanda lilinipa exposure kubwa sana.
Baada ya kuniona, baadhi ya wadau wa masuala ya mitindo,
walinishauri niingie kwenye mitindo.
So show ya Rwanda Cultural Fashion ilipoanza, mwaka 2013 nilijiandikisha na kushiriki na kufanya vizuri sana.
Niliingia
kwenye modeling ili niweze kublend it na business. Nina ndoto za
kuwa mfanya biashara mkubwa, ndio maana ninasoma biashara pale
University Of Kigali
Hope
anawashauri wanamitindo wafanye kazi kwa kujituma na wawe
wajanja wa kutafuta na kuzitumia fursa mbalimbali za mitindo,
kwani modeling ni kazi kubwa yenye fursa nyingi sana za
kibiashara.
Ana
amini kuwa kujulikana “ exposure’ ni hatua kubwa sana kwa
mwanamitindo kuweza kupata nafasi ya kupata deals na endorsements
Pamoja
na kwamba, ana ndoto za kuwa mfanyabishara mkubwa, lakini ana
amini pesa si kila kitu. Kwake yeye kuwa na hekima ni bora
kuwa na pesa na mali nyingi. “ Maarifa hudumu daima milele
lakini, pesa na mali huweza kuisha na kutekeketea wakati wowote.
Akitoa
maoni na mtazamo wake kuhusu wanaume anasema “ Wanawake hatuwezi
kuishi bila wanaume. Vile vile, wanaume hawawezi kuishi bila
wanawake. Hii ndio sababu Mungu aliwaumba Adam na Eva
Kuhusu aina ya mwanaume anaye mpenda , Hope anasema :
“
Napenda niwe na mwanaume ambaye hanipangii aina ya mavazi ya
kuvaa. Pesa na muonekano, havina umuhimu wowote kwangi, ili mradi
tu ninaishi maisha huru ya bila kuwa na stress. “
Kuhusu
aina ya kifo ambacho atapenda afe, Hope anasema, “ hakuna mtu
asie ogopa kufa, lakini si njambo baya kuomba kifo chema, na mimi
katika hilo, ninamuomba Mungu, siku yangu ikifika nife nikiwa
usingizini.
Kuhusu
asicho kipenda, Hope anasema hapendi uchafu,. Anachukizwa sana na
uchafu. Usafi ndio kila kitu kwangu, hata nilipo kuwa Fawe
Girls, nilipewa cheti cha kuwa mwanafunzi msafi.
Mbali
na mitindo, Hope anajishughulisha na kazi mbalimbali za kijamii,
huku akipenda zaidi kuwasaidia watu w asio jiweza na wanaoishi
katika mazingira magumu.
“
Huwa ninafarijika sana moyoni, ninapo ona mtu Fulani amelala
usingizi mzuri na wa amani, kwa sababu ya msaada nilio mpa.
Post a Comment