Ommy Dimpoz afanikisha uzinduzi wa video yake
Ommy Dimpoz akiongea jambo wakati wa sherehe za uzinduzi wa video ya wimbo huo.
Mrembo aliyewahi kushiriki kwenye Big Brother Africa enzi hizo Abby akimpa kampani Ommy Dimpoz kwa kucheza kwenye uzinduzi huo.
Vanessa
Mdee akiwa kwenye pozi mara baada ya kuwasili ukumbini hapo.
Wasanii
wa Bongo Fleva Joh Makini na Ben Pol wakiwasili ukumbini hapo.
Baadhi
ya warembo waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo wakiwa katika pozi.
Christian Bella akiimba kwenye uzinduzi huo.
Mtangazaji
wa Clouds FM Millard Ayo akimhoji jambo mmoja wa wasanii wa Bongo Fleva, Madee.
Ommy Dimpoz akimshukuru Bella wakati akiimba kama moja ya kumsapoti.
Baadhi
ya mashabiki waliohudhuria ukumbini hapo wakifuatilia kwa makini zoezi la
uzinduzi huo.
STAA
wa Bongo Fleva, Omari Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, usiku wa kuamkia leo alifanikisha
uzinduzi wa kichupa cha wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Achia Body.
Uzinduzi
huo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Akemi uliopo ndani ya jengo la Golden Jubilee
Tower, ambapo ulihudhuriwa na baadhi ya wasanii wenzake kibao.
Wasanii
waliojitokeza kumpa nguvu Ommy Dimpoz ni pamoja na Joh Makini, Ben Pol, Chege, Madee,
Vanessa Mdee, Navy Kenzo Christian Bella na Mwana FA.









Post a Comment