Nay Wa Mitego Atembelea Global TV, Afunguka Mimba ya Nisha!
MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma yake ya Sijiwezi, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego‘ ameweka wazi kuhusu skendo inayosambaa mitaani kuhusu ‘ujauzito’ aliokuwa nao aliyekuwa mpenzi wake, Nisha kwamba si lolote, alifanya hivyo kwa kutafuta kiki tu.
Akizungumza hayo ndani Global Tv Online, Nay alisema kuwa msichana huyo aliamua kufanya hivyo kwa sababu tu kulikuwa na kitu anakitafuta na si kwamba alikuwa na mimba kama alivyokuwa akidai.
“Wengine walisema ni yangu, si kweli, sikuonana naye kwa miaka miwili, ilikuwaje mimba iwe yangu? Maneno hayo yalinihuzunisha, nilikuwa nasoma mitandaoni, natajwa mimi mtu ambaye sikuhusika kwa lolote lile. Kuna kitu alikuwa akikitafuta, labda kiki, sijui ila watu wajue kwamba sihusiki chochote na ule ujauzito bandia,” alisema Nay.
Mbali na suala la ujauzito wa Nisha, pia Nay alilizungumzia bifu lake na Prodyuza T-Touch kwa kusema kuwa hana bifu naye au kama prodyuza huyo ana bifu naye lakini anachokiangalia ni mambo yake ya muziki tu.
“Sina bifu na T-Touch, labda awe na bifu nami. Nilifanya mambo mengi kwa ajili yake, nilijitoa kumtangaza, tulifanya kazi vizuri kwa kipindi kirefu, kuhusu kugombana, hutokea lakini kwangu, kwa kweli sina bifu naye, au yeye awe na bifu nami,” alimalizia Nay.
VANESSA MDEE ASEMA JUX NI DUME SURUALI MSIKILIZE!
Post a Comment