Tundu Lissu Afunguka Baada ya Kutembelwa na Katani Ahmad Katani, mbunge wa Jimbo la Tandahimba
Mbunge
wa Singida Mashariki kwa tiketi ya (CHADEMA) Mhe. Tundu Antiphas Lissu
amefunguka na kusema amefarijika sana kutembelewa na Mbunge wa
Tandahimba (CUF) Katani Ahmad Katani na kudai mbunge huyo alikuwa
miongoni mwa watu waliompeleka Nairobi.
Lissu
ameeleza hayo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii na kusema mbali
na kumlijua hali lakini waliweza kujadiliana kuhusu mwenendo wa siasa
zinazoendelea nchi Tanzania.
"Mheshimiwa
Katani amekuja Ubelgiji kunijulia hali pamoja na kuja kujadiliana nami
masuala mbali mbali yanayohusu siasa za nchi yetu na mustakbali wa Taifa
letu. Katani alikuwa kwenye msafara wa Wabunge walionipeleka Nairobi,
Kenya, mara baada ya jaribio la mauaji la September 7, na alikaa Nairobi
kwa siku nne. Nimefarijika sana na ugeni huu wa ndugu yangu na kaka
yangu Katani", amesema Lissu.
Mbunge
Tundu Lissu alishambuliwa na watu wasiojulikana tangu Septemba 7,2017
akiwa mkoani Dodoma, na kisha kupelekwa nchini Nairobi kwa matibabu na
baada ya miezi 3 alipelekwa nchini Ubelgiji kwa hatua nyingine ya
matibabu.
Post a Comment