CHADEMA Watoa Kauli Baada ya Mbowe Kutajwa Kwenye Orodha ya Makonda..!!
Muda mchache baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda
kutangaza majina ya baadhi ya watu wanaotuhumiwa kuhusika katika mtandao
wa biashara ya Madawa ya kulevya akiwemo kiongozi ya juu wa CHADEMA na
kambi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe, Uongozi wa CHADEMA umefunguka
na kueleza namna ambavyo hawakupendezwa jinsi jina la kiongozi wao wa
juu lilivyotajwa bila kufuata utaratibu.
Wakizungumza na waandishi wa habari Jumatano hii, CHADEMA wamedai wao
hawapingi kutajwa kwa mkuu wao ila wanapiga utaratibu iliyotumika kutaja
jina la kuingozi huyo wa juu wa chama hicho.
“Kimsingi katika majina mengi yaliyotajwa kuna jina la Mwenyekiti wa
chama Mbowe, swala la utetezi wake au maelezo hilo ni swala binafsi
sababu kilichotajwa ni jinai lakini kimsingi tunachukua nafasi hii
kulaani,” alisema mmoja kati ya viongizi hao.
“Tunalaani jinsi tusivyoweza kuendesha utawala wa sheria kwenye nchi
yetu na jinsi tusivyofata kanuni zilizowekwa dhidi ya sheria, Mh. Mbowe
ni kiongozi wa kitaifa, ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni,
ni Mbunge wa Hai…. kwahiyo kuna taratibu za kufata unapokua na kusudio
la kumuita,”
Aliongeza, “Kitendo cha kwenda kuongea kwenye mkutano na Waandishi wa
habari na kutaja viongozi wakuu wa kitaifa ambao wana tuhuma tu ambazo
hazijathibitishwa, ni kukosa ustaarabu wa kiuongozi, tusingependa kuona
viongozi wengine waandamizi kutendewa kama alivyotendewa kiongozi wa
chama chetu,”
Pia katika list hiyo mpya ya Makonda ametajwa aliyekuwa Mbunge wa CCM, Iddi Azzan, mchungaji Gwajima pamoja na watu wengine.
Post a Comment