MADEGA ASIMULIA MWANAYE ALIVYOGONGA WATU NA BAADAYE KUWAWA AKIKIMBILIA DAR

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Imani Madega amesimuliwa namna alivyopata msiba mkubwa wa kufiwa na mwanaye.
Mwanaye
huyo anaitwa Omary Madega na amefariki baada ya kupata ajali akiwa
anaendesha gari la Madega akijaribu kuwakimbia madereva bodaboda.
Omary
anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 32, aliuawa wakati akiwakimbia
bodaboda katika eneo la Chalinze mkoani Pwani akiwa anatumia gari la
baba yake mdogo, Madega ambaye kitaalamu ni mwanasheria.
Akizungumza
na Championi Jumatano, Madega aliyeonyesha masikitiko makubwa alisema
gari lililosababisha ajali ni Mitsubushi Pajero, mali yake.
“Nina
msiba mkubwa sana ndugu yangu. Nilisafiri kutoka Dar es Salaam hadi
Chalinze ambako nilipitiliza kwenye project yangu. Nikiwa huko gari
lilisumbua.
“Nikamuita
Omary ambaye ni mtoto wa kaka yangu aje alishughulikie. Alipofika pale
alikuwa na fundi, akamchukua na mtu ambaye amekuwa akisimamia nyumba
yangu ninapokuwa Dar es Salaam pamoja na Shamba Boy wangu.
“Wote
wanne waliondoka kwenda kuifuata gari nilipoiacha. Walipofika haikuwa
na tatizo kubwa, kawaida ikishapoa huwa inawaka, basi wakaichukua. Sasa
si unajua vijana, wakaona waingie mtaani kidogo.
“Kama
dakika 10 tokea waondoke, nikapigiwa simu kwamba Omary kagonga watu
watatu pale sheli na inasemekama mmoja amepoteza maisha na alikuwa
anabishana na madereva bodaboda. Mwisho aliondoa gari kasi kama
akiendelea Dar es Salaam.
“Dakika
5 baadaye sijajua hata cha kufanya, nikapigiwa simu ile gari imepata
ajali na Omary amefariki dunia pamoja na yule mtunza nyumba,” alisema
Madega.
Kwa Mujibu Madega Omary amezikwa Jumapili, mtunza nyumba wake kazikwa juzi na mchungaji wake bado ana hali mbaya katika hospitali ya Tumbi kwa kuwa mguu wake umevunjika vibaya na unahitaji upasuaji.
Post a Comment