Chirwa Ashangaa Milioni 150 za Yanga
BAADA ya kuwepo kwa taarifa mbalimbali zikimhusu straika wa Yanga,
Obrey Chirwa raia wa Zambia kugoma kuichezea timu hiyo, mwenyewe
ameibuka na kutoa msimamo wake ndani ya timu hiyo.
Chirwa aliyejiunga na Yanga msimu uliopita akitokea FC Platinum ya Zimbabwe, mkataba wake na Yanga unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu huku kukiwa na taarifa za Simba kuinyemelea saini yake.
Hivi karibuni, taarifa zilitoka zikidai kwamba, Mzambia huyo ametaka kupewa kitita cha shilingi milioni 150 ili aongeze mkataba ndani ya timu hiyo.
Taarifa za Chirwa kugoma kuichezea Yanga, zilianza wikiendi iliyopita baada ya jina lake kuondolewa dakika za mwisho kwenye msafara wa timu hiyo ulioelekea Shelisheli kucheza mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St Louis.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0, ambapo kwenye mchezo huo, Chirwa alikosa penalti, huku Yanga ikifunga bao lake hilo kupitia kwa Juma Mahadhi.
Kuachwa kwa Chirwa kwenye msafara huo, kulitolewa ufafanuzi na Yanga kwa kusema kuwa, mchezaJi huyo alipata majeraha kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Majimaji ambao Yanga walishinda mabao 4-1.
Baada ya kuenea taarifa za kugoma kwa Chirwa, juzi Jumatatu klabu hiyo iliweka katika akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Instagram sehemu ya mahojiano na Chirwa.
“Sijawahi kusema wala kumwambia mtu yeyote kuwa nataka 150M kwa ajili ya mkataba mpya, sipendezwi na namna wanavyonizushia, nadhani nia yao ni kunigombanisha na wapenzi wa Yanga.
“Niliumia kwenye mchezo dhidi ya Majimaji, ajabu wanasema nimegoma, huu ni upuuzi, mimi ni mchezaji wa Yanga, mimi na klabu ndiyo wenye kujua hatima yangu ya baadaye, niacheni nicheze mpira,” alisema Chirwa.

Post a Comment