LOGARUSIC AENDELEA KUPIGA MISHEMISHE ZA KUTAKA KUREJEA BONGO
Kocha
Mkuu wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic ‘Loga’ raia wa Croatia,
ameibuka na kusema kuwa bado anaipenda Tanzania, hivyo anatamani siku
moja arudi kufundisha moja kati ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara.
Loga
ambaye alijiunga na Simba Desemba, 2013 na kupewa mkataba wa miezi sita
uliomalizika mwishoni mwa msimu wa 2013/14 kabla ya kuongezewa mwaka
mmoja, kwa bahati mbaya hakumaliza mkataba wake huo mpya, akatimuliwa
baada ya kuutumikia kwa takriban wiki tatu kwa kile kilichoelezwa ni
kutofautiana na viongozi wake.
Kocha
huyo ambaye hivi karibuni amemaliza mkataba wake wa kuinoa Interclube
ya Angola, siku chache kabla ya mkataba wake huo kumalizika, alifanikiwa
kuiongoza kubeba ubingwa wa kombe la chama cha soka cha nchi hiyo
(APFL) baada ya kuinyuka Petrol mabao 3-0.
“Kwa
sasa nipo Croatia baada ya mkataba wangu kumalizika kule Angola, sina
timu na nafanya mpango wa kupata sehemu nyingine ya kufundisha,
matarajio yangu makubwa ni kuja tena Tanzania kufundisha, kwani bado
napapenda.
“Nimeachana
na Interclube baada ya kuinoa kwa siku 284 na kucheza mechi 39 nikiwa
kama kocha mkuu, sina budi kuwashukuru Waangola kutokana na ushirikiano
walionipa kwa wakati wote niliokuwa kwao,” alisema Loga.

Post a Comment