Umeshajua unapendwa, unatikisa kiberiti ili iweje?
Mada ya leo, kuna kawaida ambayo si rasmi imejijenga kwa mtu akishagundua anapendwa. Anajaribu kumtikisa mwenzake ili kupima tu ule upendo kutoka kwa mwenzake. Anajaribu kufanya jambo ambalo anajua kabisa hata haliwezekani katika hali ya kawaida, yeye atafanya tu ili aone utasemaje.
Tabia hii ipo kwa wanawake na wanaume
lakini zaidi hufanya na wanawake. Mwanamke anakuwa anajua anapendwa,
anatambua mpenzi au mume wake anampenda lakini anajaribu kumchokonoa ili
kuona kama anapendwa kweli. Hiyo ndiyo furaha yake.
Mfano, anaweza kumuambi; ‘mbona kuna mtu
kaniambia amekuona baa ukiwa na mwanamke.’ Anauliza swali hilo akiwa
anajua kabisa si kweli. Anajua shughuli za mpenzi wake za kila siku
namna ambavyo zinambana.
Hajakaa sawa, anajua mpenzi wake
amechoka lakini badala ya kumpa pole ya kazi na kumfariji kwa namna
inayofaa, anamuambia; ‘naomba ukanichotee maji bombani.’
Huo ni mfano tu. Mwanamke huyo anakuwa
haumwi, mzima wa afya. Anatambua fika mpenzi wake amechoka kwa wakati
huo lakini anamjaribu hivyo ili asikie atajibu nini.
Anaweza kujua kwamba mpenzi wake hapendi kitu fulani, kwa makusudi anakifanya hicho kitu ili kuona mpenzi wake atachukua hatua gani.
Anaweza kujua kwamba mpenzi wake hapendi kitu fulani, kwa makusudi anakifanya hicho kitu ili kuona mpenzi wake atachukua hatua gani.
Hao ndiyo wanawake. Kwa upande wa wanaume pia wapo wa aina hiyo.
Akishagundua anapendwa, anaanza kutikisa kiberiti kwa kumjibu vibaya mpenzi wake. Anafanya vile akiamini kwamba kwa vile mpenzi wake anampenda sana, hawezi kufanya lolote. Analeta pozi tu makusudi moyoni akitoa kauli za ‘hapindui huyu…ameshakolea kwangu.’

Marafiki zangu, hapa lazima tujifunze
kitu! Ukiona unapendwa sana na mwenzako, unapaswa kurejesha upendo kama
au zaidi ya huo unaooneshwa na mwenzako. Unapaswa kuthamini penzi la
mwenzako kwa hali na mali. Huna sababu ya kutikisa kiberiti, unaweza
kufanya hivyo halafu ikawa ugomvi mkubwa utakaosababisha akuchukie
kabisa.
Kumtikisa mwenzako siyo sifa. Umeshajua
mwenzako anakupa upendo wa dhati, kwa nini na wewe usimuoneshe kama
unampenda? Mapenzi ni hiari, kama mlikubaliana, mkapeana mikakati yenu,
kwa nini msumbuane kwa vitu vya kipuuzi? Faida ya kuishi kwa amani na
furaha katika uhusiano si ya mtu mmoja bali ni yenu wote.
Kama mmepanga safari ya kuelekea kwenye
ndoa, hakuna haja ya kupimanapimana. Msichezeane hisia. Wewe mwenzako
anakuwa ameshawekeza nguvu, akili na upendo wake, usimtafutie ‘visababu’
vya ajabu vitakavyosababisha ugomvi kila wakati.
Kwa leo ni hayo, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri ya kusisimua!
Kwa leo ni hayo, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri ya kusisimua!

Post a Comment